Kwa kuzingatia Kifungu cha 44(5)
cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ikisomwa
pamoja na Kanuni ya 28(1)(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
(Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea
Rufaa kumi na tano (15) kutoka kwa Wagombea Udiwani wa Halmashauri
mbalimbali zenye Uchaguzi Mdogo wa Madiwani.
Kati ya Rufaa hizo kumi na tano
(15), Rufaa 9 ziliwasilishwa na Wagombea ambao hawakuridhishwa na
maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi waliowaengua kutoka katika orodha ya
wagombea wa Udiwani katika Kata mbalimbali.
Aidha, Kati ya Rufaa kumi na tano
(15), Rufaa sita (6) ziliwasilishwa na Wagombea ambao hawakuridhishwa
na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi ya kuwaruhusu wagombea wenzao
kuendelea kugombea udiwani katika Halmashauri mbalimbali.
Kuanzia tarehe 03 hadi 04
Novemba, 2017, Tume kwa mujibu wa Kanuni ya 29 ya Kanuni za Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015, ilipokea,
ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa hizo. Yafuatayo ndiyo maamuzi ya
Tume:
Kuhusu Rufaa tisa (9) za wagombea
waliokata Rufaa kupinga maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi kuwaondoa
katika kugombea Udiwani, Tume imekubali Rufaa zao na kuwarejesha katika
kugombea udiwani katika Kata husika kuanzia tarehe ya leo 04 Novemba,
2017.
Kuhusu Rufaa sita (6) za wagombea
waliokata Rufaa kupinga maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi ya kuwaruhusu
wagombea wenzao wa Udiwani kuendelea na Kampeni za Udiwani, Tume
imezikataa Rufaa na imekubaliana na Maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi.
Hivyo, wagombea sita (6) waendelee kuwa wagombea.
Taarifa rasmi za maamuzi ya Tume zimetumwa kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili wawapatia wahusika maamuzi ya Tume.
Imetolewa leo tarehe 04 Novemba, 2017 na;
No comments:
Post a Comment