MKUU wa mkoa wa Pwani,mhandisi
Evarist Ndikilo ,akizungumza na wadau wa korosho katika kikao cha
tathmini na maandalizi ya msimu mpya wa zao hilo la
biashara,kilichofanyika Mkuranga.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo
………………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
WADAU wa zao la korosho mkoani
Pwani ,wamekubaliana kwa pamoja kila kilo moja ya korosho itakayouzwa
msimu huu ,itakatwa shilingi.20 kwa ajili ya kuchangia sekta ya elimu
mkoani humo .
Katika msimu wa korosho 2016/2017
wadau hao waliazimia ikatwe shilingi tano kwa kila kilo kiasi ambacho
kimeonekana hakitokidhi mahitaji.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
baadhi ya wajumbe wa kikao cha tathmini na maandalizi ya msimu mpya wa
korosho,akiwemo mzee Juma Mkwanywe,kilichofanyika Mkuranga,walisema zao
hilo ni la biashara hivyo linaweza kuwainua katika kutatua changamoto
zinazowakabili kielimu .
“Zipo bado changamoto nyingi za elimu ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ,shule chakavu na kuongeza madarasa”
“Kiasi hiki sio kidogo hata
kidogo ,kwani tukichukulia msimu wa 2016/2017 ziliuzwa tani 13,257,856
kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani “
“Sasa tani zote hizo tungetoa shilingi 20 kwa kila kilo tungekuwa na mamilioni mangapi ya fedha” alieleza.
Mkwanywe alielezea elimu ni jambo
muhimu kwa watoto hivyo endapo wakitekeleza maamuzi yao itasaidia
kupunguza baadhi ya kero hizo.
Hata
hivyo alisema kuwa ,inawezekana kukawepo sheria zinazokataza kutoa
fedha hizi za wakulima kufanya jambo kama hilo lakini kutokana ni
maamuzi ya umoja hakuna kitakachopingika .
Aidha wadau hao wameazimia pia minada inayotarajiwa kuanza novemba 8 iwe inafunguliwa mapema.
Hata hivyo ,walisema wataalamu wa ubora waongezwe na elimu ya matumizi ya dawa itolewe kwa wakulima .
Madai
ya watoaji huduma yakapelekwe bodi ya korosho mapema ili kupata fungu
lao na vitini vya taarifa vipelekwe kwa wajumbe ili wakapatiwe na
wakulima wengine kujua kinachoendelea .
Baada ya wadau hao kuazimia mambo
hayo kwa umoja wao ,mwenyekiti wa kikao hicho,ambae pia ni mkuu wa mkoa
wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo alisema mkakati wa serikali ya awamu
ya tano ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwenye mazingira bora.
Alielezea ipo baadhi ya mikoa
iliyonufaika na mazao ya biashara ya mikoa yao ikiwemo kahawa mkoani
Kilimanjaro ,Kagera ,Mbeya na pamba katika kanda ya Ziwa sanjali na miwa
mkoa wa Morogoro .
Mhandisi Ndikilo alisema inawezekana zao la korosho likainua uchumi na kutatua matatizo yaliyopo mkoani humo.
“Tumekubaliana kwa umoja wetu
kutenga sh.20 kwa kila kilo moja ya korosho itakayouzwa katika msimu huu
naamini tutafanikiwa kupambana na changamoto mbalimbali zinazotukabili
kwenye elimu”alisema mhandisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo aliwataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuimarisha ulinzi kwenye vizuizi kudhibiti utoroshaji wa korosho .
Alisema msimu huu hawana simile
kwa wale watakaobainika kutumia mifumo isiyo rasmi zaidi ya mfumo wa
stakabadhi ghalani ambapo aliwataka wakulima kuanika korosho zao ili
ziwe na ubora .
Mkuu huyo wa mkoa alihimiza kufufuliwe mashamba ya mikorosho ,na kupalilia mwezi January badala ya mwezi June .
Mwisho
No comments:
Post a Comment