Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza wakati wa mkutano wa utambuzi wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga wilayani mufindi mkoani Iringa
Prof Aldo Lupala akitambulisha na kuelezea jinsi gani walifanikiwa kuundaa mpango huu kwa tija na maendeleo ya halmashauri ya mji wa mafinga
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza sambamba na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri williamu wakati mkutano wa utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga
Na Fredy Mgunda, Iringa
Halmashauri ya mji wa
mafinga wilayani mufindi mkoani Iringa yajipanga kuwa manispaa kwa kuanza
kuupanga mji kuwa wa kisasa na wakibiashara kwa kutumia wataalamu kutoka chuo
cha SUA na wataalamu kutoka halmashauri hivyo.
Akizungumza wakati wa kikao
cha mpango kabambe wa mji wa mafinga mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema
kuwa mji wa mafinga unatakiwa kukuwa kwa mpangilio unao stahili hivyo kuanza na
mpango huu itakuwa njia mbadala ya kutatua changamoto mbalimbali za miundo
mbinu ambazpo mikoa mingine kuna migogoro mingi.
“Niwashukuru wataalamu na
viongozi wa halmashauri hii kwa kazi kubwa mliyoifanya ya kubuni na kuanzisha
mpango kabambe ambao utakuwa mfano kwa halmashauri nyingine zinazokuwa kwa
kasi na hazina mpango kama huu” alisema Masenza
Masenza aliwataka viongozi
na wadau wa maendeleo katika halmashauri hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa
wananchi juu ya mpango huo kabambe ambao utasaidia kukuza mji kwa kasi na kuwa
na mpangilio unaotakiwa hapa nchi.
“Sasa naona tuliopo hapa
tunatosha kufikisha ujumbe huu kwa wananchi na wadau wengine ambao
hawajahudhuria mkutano huu ili jamii kuwa na elimu na kuondoa migogoro na minong’ono
iliyopo kwa wananchiwasiojua chochote kuhusu mpango huu” alisema Masenza
Aidha masenza aliwashukuru
wataalamu kutoka chuo SUA kwa kufanikisha mpango kabambe huo kwa gharama nafuu
tofauti wangepewa makampuni binafsi ambao mara nyingi gharama zao huwa juu sana
tofauti na taasisi za kiserikali na kuitaka halmashauri ya mji wa mafinga
kuendelea kuzitumia taasisi za kiserikali zenye uwezo na vigezo stahili kweli
miradi mbalimbali ya mji wa mafinga.
Kwa upande wake mwenyekiti
ya halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga alisema kuwa mpango kabambe huu
utadumu kwa takribani miaka hamsini ijayo hivyo wakazi wa halmashauri hiyo
watanufaika kwa kuwa na mji ambao utakuwa umepangiliwa kwa kila kitu.
“Mkuu wa mkoa nikuahidi kuwa
mpango huu utakuwa wa miaka mingi na tutafuata mambo mazuri yote kutoka kwa
wataalamu ili kuufanya mji wa mafinga kuwa kivutio cha miji mingine na
kuwafanya watu wenngine kuiga mfano kutoka kwetu” alisema Makoga
Makoga aliwapongeza
wanafunzi, wataalamu wa chuo cha SUA pamoja na wataalamu kutoka halmashauri kwa
kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kuhakikisha mpango huo kukamilika kwa wakati
pasipo kuwa na changamoto zozote zile.
Halmshauri ya mji wa mafinga
tunategemea hivi karibuni kuwa manispaa kwa kuwa vigezo karibia vyote tunavyo
hivyo tunaomba kuendelea kushirikiana na kushauriwa katika mikakati ya kuukuza
mji huu unakabiliwa na ongezeko la watu kila siku alisema Makoga.
Naye prof. Aldo Lupala alisema
kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na wataalamu wengi hivyo ni vyema wakatumiwa
katika miradi mingi ya kimaendeleo ili kungeza ajira na kukuza ujuzi wao pindi
wawapo kazini.
“Unajua ukiwa mtaalamu
halafu huna kazi kwa kiasi fulani utaalamu au ujuzi wake utapungua toafuti kila
wakati mtaalamu akiwa kazini huongeza ubunifu na kukuza utaalamu wake hivyo
mgeni rasmi naomba tufikishie ujumbe huu serikali kuu” alisema Lupala
Prof Lupala aliupongeza
uongozi wa halmauri ya mji wa mafinga kwa kufanya kazi na wataalamu kutoka chuo
kikuu cha SUA kwa ushirikiano mkubwa ambao umefanikisha kupata mpango kabambe
ambao utaisaidia halmashauri kwenye mipango ya kuukuza miji huo wa mafinga kuwa
manispaa.
No comments:
Post a Comment