Miongoni mwa watu wetu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali katika miili yao bila kujua hasa nini chanzo.
Hata
hivyo wengi wao pia hupenda kujua nini kinachowasumbumbuwa lakini uwezo
wa kifedha kuwa mdogo wakati mwingine umekuwa ni chanzo kikubwa kwao
hasa inapofikia muda wa kupata huduma za vipimo sahihi hospitalini.
Serikali
ya Tanzania kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam imetoa siku 5
kwa wananchi wa Mkoa wa Huo kujitokeza siku ya jumatano tarehe 6
Septemba mwaka huu katika viwanja mnazi mmoja ,kupima afya zao.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ambapo
amesema serikali yake imeona ni vyema kuendeleza huduma ya afya, hivyo
wananchi wote wa mkoa huo wametakiwa kujitokeza kuanzia asubuhi mpaka
jioni kupima ili kujua afya zao.
“Kitendo
cha kupima afya kinatoa unafuu wa kujua namna gani ya kujipanga katika
sekta nzima ya afya ilikupunguza vifo,kuna magonjwa mengine ambayo
huwezi kuyafahamu mpaka upimwe alafu ugundulike kinachokusumbua,na
wakati mwengine ukichelewa kupatiwa huduma, huwapa shida kubwa madaktari
na hata wewe mwenyewe unaweza kupoteza maisha yako kwa kuchelewa kujua
kinachokusumbua”Alisema Makonda.
Ameleeza
kitendo hiki kinamhamasisha mwananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya
ambapo kufanya hivyo kunarahisisha kuepusha gharama, na kuondokana na
Magonjwa ambayo ungeweza kuyaepuka endapo utapata taarifa mapema.
Magonjwa yatakayopumwa ni pamoja na kansa,tezi dume,macho,meno,na kila aina ya ugonjwa .
Aidha
Makonda amesema kutokana na changamoto ya ugonjwa wa homa ya ini ,
madaktari wanajipanga kuona namna gani wanaweza kushughulika na ugonjwa
huo.
Amefafanua
kuwa lengo lake ni kuona hakuna mwananchi ambao watakufa kwa kukosa
huduma ya afya isipokuwa mgonjwa afe kwa mapenzi ya Mungu.
Upimaji
huo utakuwa ni bure bila tozo ya aina yeyote,ambapo wataalamu zaiidi ya
mia mbili watakuwa tayari kwa kutoa huduma kwa wananchi watakao
jitokeza.
Nae
Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Grace Magembe amesema zoezi
hilo limeshirikisha wadau kutoka serikalini na wengine wa taasisi
binafsi ambapo kwa upande wa Serikali, madktari kutoka hospitai ya
Taifa Muhimbili Jakaya Kikwete, Ocean Road, Amana, Mwananyamala, Temeke,
wengine ni TMJ, LEGENCY, AGAKHAN, IMILIFE, Chama cha watoa huduma
binafsi, CCP MEDICINE, DAMU SALAMA, Shirikaa la MDH, Shirika la bima ya afya
NHIF, KAIRUKI, SANITAS.N.K
Amesema wagonjwa wote watahudumiwa na wale watakao stahili kupata rufaa atapewa kuwakati unaotakiwa.
No comments:
Post a Comment