Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya
Fedha na Mipango – Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy (wa tatu kutoka
kushoto, mwenye tai nyekundu) na kiongozi wa ujumbe kutoka Taasisi ya
Kimataifa ya Kupunguza Umaskini China, Bw. Xia Gengsheng (wanne kutoka
kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka China na
viongozi wa Tume ya Mipango.
Wataalamu kutoa Tume ya Mipango
wakiwa katika kikao na Ujumbe kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kupunguza
Umaskini China (hawapo pichani).
Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya
Fedha na Mipango – Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy (katikati), Naibu
Katibu Mtendaji, Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi
Bw. Paul Sangawe (kulia) na Kaimu Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia
Klasta ya Huduma za Jamii na Idai ya Watu, Tume ya Mipango, Bw. Ibrahim
Kalengo (kushoto) wakimsikiliza mjumbe (hayupo pichani) kutoka China
wakatika wa kikao.
………………………..
Na Adili Mhina
Taasisi ya Kimataifa ya Kupunguza
Umaskini China (IPRCC) imeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano
baina yake na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Tume ya Mipango kwa
lengo la kuongeza kasi ya maendeleo na kupunguza umaskini nchini.
Uamuzi huo umefikiwa katika kikao
cha wataalamu kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango kupitia Tume ya Mipango
wakiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji Bw. Maduka Kessy na ujumbe kutoka
taasisi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao hicho
kiongozi wa ujumbe kutoka China Bw. Xia Gengsheng alieleza kuwa maeneo
mapya yanayotarajiwa ni pamoja na kuanzisha vituo vingingine vya mfano
vya kilimo katika vijiji mbalimbali hapa nchini.
Bw. Xia alieleza kuwa wameamua
kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano kutokana na mafanikio
yaliyojitokeza katika juhudi za kupambana na umaskini nchini hususan
katika kutoa elimu ya kilimo kwa wakulima kupitia kuanzishwa kwa Kijiji
cha mfano cha Peapea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
“Ndugu Kaimu Katibu Mtendaji
naomba nikuhakikishie kwamba tutaanzisha vijiji vingine vya mfano kama
kile cha Peapea na kutoa fursa kwa wananchi wengi zaidi kujifunza mbinu
bora za kilimo ili waweze kuendesha kilimo chenye tija na waondokane na
umaskini,” alieleza Bw. Xia.
Eneo jingine la ushirikiano
litakalo anzishwa ni masuala ya utafiti ambapo IPRCC kwa kushirikiana na
Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Tume ya Mipango na taasisi zingine
itawezesha kufanyika kwa tafifi katika kuchochea maendeleo na kutafuta
mbinu mbalimbali za kupunguza kasi ya umaskini.
Kwa upande wake Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy alieleza kuwa ushirikiano
kati ya Tume ya Mipango na Taasisi ya IPRCC ambao umedumu kwa zaidi ya
miaka sita umekuwa na faida kubwa katika kukabiliana na umaskini kwa
watanzania.
Alielezea kuwa kwa kipindi hicho
Tume ya Mipango na IPRCC wamefanikiwa kuendesha programu mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuratibu mazungumzo ya kisera juu ya mageuzi ya
kilimo vijijini na kupunguza umaskini, kuanzishwa kwa kituo cha mfano
katika kupunguza umaskini kwa wakulima wadogo Kilosa Mkoani morogoro.
Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya
Tume ya Mipango na IPRCC umefanikisha uratibu wa programu za
kuwajengea uwezo watanzania kwa kutoa udhamini wa masomo katika ngazi za
uzamili na uzamivu katika fani za maendeleo vijijini pamoja na kuandaa
mafunzo mbalimbali yanayohusu mageuzi ya kilimo kwa maafisa kilimo
pamoja na wakulima wenyewe.
Pamoja na mambo mengine, Taasisi
ya Kimataifa ya Kupunguza Umaskini ya China imekuwa ikisaidia kutoa
msaada wa kitaaalamu ambapo wataalamu wa kilimo kutoka China wamekuwa
wakitoa mafuzo kwa wakulima mkoani Morogoro.
No comments:
Post a Comment