Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa, anatarajia kuongoza
kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa siku mbili Jijini Dar es
Salaam, Septemba 30 hadi Oktoba 1, 2017.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Septemba 24 na Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole ameeleza kuwa, Kamati kuu ya
Halmashauri ya Taifa (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vinatarajia
kuketi Jijini Dar e Salaam kwa nyakati tofauti.
No comments:
Post a Comment