Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga ametua nchini katika mkutano wa majaji na mahakimu akionekana kivutio kwa wengine.
Jaji
huyo ni mmoja wa majaji wakuu 13 kutoka nchi mbalimbali duniani
wanaohudhuria mkutano majaji na mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola
unaofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku tatu..
Maraga
amegeuka kivutio baada ya kushangiliwa na majaji waliohudhuria mkutano
huo wakati alipotambulishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim
Juma.
Profesa Juma amempongeza Maraga kwa kuwakilisha mfano bora wa kulinda uhuru wa Mahakama kwa nchi nyingine duniani.
Kiongozi huyo ameonekana akiwa ameambatana na walinzi wanne ambao wanamfuata popote anapotembea nje ya mkutano huo.
Hata
hivyo, Maraga amekataa kuzungumza na vyombo vya habari kwa madai
amekuja kuhudhuria mkutano huo na siyo kwa jambo jingine lolote.
Mkutano
huo umefunguliwa leo Jumatatu na Makamu wa Rais, Samia Suluhu ukiwa na
kauli mbiu "Kujenga Mahakama Shirikishi, Thabiti na Inayowajibika."
Jaji
Maraga kwa siku za hivi karibuni amekuwa maarufu baada ya kutoa uamuzi
wa kufuta Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliokuwa umempa ushindi Rais Uhuru
Kenyatta.
No comments:
Post a Comment