Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA,
umesema siku ya Jumanne utaongoza maandamano ya wafuasi wake nje ya
Ofisi ya Tume ya Uchaguzi jijini Nairobi, kushinikiza mabadiliko ndani
ya Tume hiyo kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi mpya wa urais tarehe 26
mwezi Oktoba.
Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga
ametangaza kuwa, hawatakubali kufanyika kwa Uchaguzi huo iwapo
Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Ezra Chiloba na maafisa wengine wataendelea
kuandaa uchaguzi mpya.
Naibu rais William Ruto ambaye pia ni
naibu kiongozi wa chama cha Jubilee ameshutumu kauli ya Odinga na
kueleza ni mbinu ya kiongozi huyo wa upinzani kutotaka Uchaguzi.
Mvutano wa kisiasa unaendelea nchini
Kenya, huku ikiripotiwa kuwa Tume ya Uchaguzi inapanga kukutanana
wawakilishi wa pande zote mbili za kisiasa, kukubaliana kuhusu
maandalizi ya Uchaguzi mpya.
Wakati uo huo, kiongozi wa mashtaka
nchini Kenya Keriako Tobiko, ameagiza kuchunguzwa kwa Tume ya Uchaguzi
nchini Kenya baada ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa urais mwezi
uliopita.
Tobiko ameagiza Polisi na maafisa wa
tume ya kupambana na ufisadi kuchunguza iwapo wafanyikazi wa Tume hiyo
waliohusika na udanganyifu uliosababisha matokeo hayo kufutwa.
Chanzo:RFI
No comments:
Post a Comment