Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa
na viongozi mbalimbali wa serikali katika ukaguzi wa jengo la Akinamama na
watoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akikagua miundombinu ndani ya jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya
Mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akikagua miundombinu ndani ya jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya
Mkoa wa Dodoma.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Charles Kiologwe akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipokuwa akikagua chumba
cha kufulia nguo za Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa
na viongozi mbalimbali wa serikali katika ukaguzi wa jengo la Akinamama na
watoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akitoa maelekezo kwa wakandarasi wa ujenzi wa jengo la Akinamama na watoto
alipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Dodoma.
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua
miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na kuahidi kuwa serikali itafanya
ukarabati wa baadhi ya majengo haraka iwezekanavyo.
Akizungumza mara baada ya kukagua miundombinu ya hospitali leo mjini
Dodoma, Jafo amesema hospitali hiyo ndio kimbilio la watu wengi na
kwamba baadhi ya majengo yake yanahitaji kufanyiwa maboresho ili yaendane na
hadhi ya Makao makuu ya Nchi.
Amesema majengo hayo yamejengwa tangu enzi za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu
Julius Nyerere ni ya zamani hivyo yanatakiwa kufanyiwa maboresho ili yawe ya
kisasa na kwamba serikali inajipanga kufanya maboresho hayo na kwa kuanzia
itapeleka Sh.milioni 500 kuanza ukarabati katika jengo la upasuaji.
Ameeleza jengo la upasuaji ni la muda mrefu na miundombinu yake kwa
ndani haiendani na hali ya sasa na kwamba inatakiwa kukarabatiwa ili iwe ya
kisasa.
“Serikali tutaleta fedha ili tukarabati jengo hili liendane na
hali halisi ya mahitaji hasa ikizingatiwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi hivyo
ni kimbilio la watu wengi,”amesema Jafo
Aidha amemuagiza
Mganga Mkuu wa Mkoa Dk.Charles Kiologwe na uongozi wa hospitali hiyo kuanza
mchakato wa kuwasilisha maombi serikalini kwa ajili ya kuboresha majengo ya
hospitali hiyo ambayo asilimia kubwa yalijengwa wakati Hayati Mwalimu Julius
Nyerere.
Kadhalika,
amepongeza ujenzi wa jengo jipya la kisasa la akina mama na watoto na kuagiza
ujenzi wake ukamilishwe kabla ya mwisho wa mwezi wa oktoba mwaka huu kwa kuwa
serikali imeshapeleka fedha za ukamilishaji.
Aidha amepongeza
ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Bima ya Afya na kwamba linapokea wagonjwa wengi
kwa siku kutokana na ubora wa miundombinu yake.
Kwa upande
wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,
Dk. Caroline Damian amesema jengo
hilo limekuwa likitumika kufanya upasuaji kwa wastani wa
watu 500 kwa wiki.
watu 500 kwa wiki.
Naye, Mganga Mkuu Dk. Kiologwe amesema miundombinu ya hospitali hiyo
ilijengwa mwaka 1929 na kwamba licha ya changamoto ya miundombinu lakini huduma
za afya zimekuwa zikitolewa kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment