Friday, August 18, 2017

Magufuli ateua maprofesa watatu kuongoza taasisi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Agosti, 2017 amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao;

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Abdulkarim Hamis Mruma kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (TIPER).

Prof. Abdulkarim Hamis Mruma ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Joseph Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Ltd.

Prof. Joseph Buchweshaija ni Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).
 
Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Evaristo Joseph Liwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (Ardhi University).
 
Prof. Evaristo Joseph Liwa amechukua nafasi ya Prof. Idrissa B. Mshoro ambaye amestaafu.
 
Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 17 Agosti, 2017

Emmanuel Buhohela
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Dar es Salaam
18 Agosti, 2017

No comments:

Post a Comment