Mti aina ya msindano ambao umegemwa
utomvu katika Shamba la miti la Sao Hill lililoko Mufindi mkoani Iringa
ikiwa ni utafiti unaofanywa na Kampuni ya Art International kwa
kushirikiana na shamba hilo ikiwa ni njia ya kujiongezea kipato(Picha na
Wizara ya Maliasili na Utalii)
Meneja wa Shamba la miti la Sao Hill,
Salehe Baleko akikinga utomvu unaotoka katika mti wa msindano ambao
baada ya kugemwa huchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali ambao
hutumika kutengenezea dawa mbalimbali ikiwemo bazoka (chewing gum)
pamoja na gel. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
Mtaalamu wa Kampuni ya Art
International, Zhoung Yhoung akitoa maelezo kuhusu zoezi la ugemaji wa
utomvu kwa ujumla unaofanywa na kampuni yake (Picha na Wizara ya
Maliasili na Utalii)
Shamba la miti la Sao Hill
likishirikiana na Kampuni ya Art International limeanza utafiti wa
kugema utomvu wa miti ya msindano kama njia ya kujiongezea kipato.
Akizungumza na Kamati ya Bunge ya
Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi ya nchini Malawi iliyotembelea
Shamba la Miti la Sao Hill, Meneja wa Shamba hilo Salehe Beleko amesema
katika kuongeza vyanzo vya mapato wameingia mkataba na kampuni hiyo
kufanya utafiti na ikibainika kwamba haitaathiri ukuaji wala ubora wa
miti wataidhinisha kuwa chanzo kipya cha mapato.
Akifafanua Salehe Baleko amesema wanatarajia kuuza kila kilo moja ya utomvu kwas h. 750.
Beleko amesema kwa kuwa ni utafiti
wameanza kwanza na miti iliyokuwa tayari kuvunwa wakiona hakuna madhara
wataendelea kwenye miti michache yenye umri mdogo na matokeo ya utafiti
huo yatapelekea ama kukuza ama kukataza kabisa zoezi hilo.
Naye mtaalamu wa kampuni ya uchina,
Yhoung Zhoung amesema taasisi yake imefuata taratibu zote za ugemaji na
usafirishaji wa utomvu huo na amefafanua kwamba kampuni yake inahitaji
miti millioni mbili kwa mwaka ilikupata ujazo wa utomvu wanauhitaji.
Akijibu swali la mke wa Rais wa zamani
wa Malawi, Patricia Muluzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ambaye
alitaka kujua matumizi ya utomvu huo mtaalamu huyo amesema baada ya
kuchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali utomvu huo hutumika
kutengenezea dawa mbalimbali bazoka (chewing gum) pamoja na gel.
Mjumbe wa Kmaati hiyo, Rashid Pemba
Msusa, amesema kwa mara ya kwanza wameshuhudia matumizi mapya kabisa ya
zao la mti teknolojia ambayo hawajawahi kuiona nchini kwao Malawi. Hata
hivyo ameahidi kufuatilia matokeo ya utafiti huo ili ukifaa wauhamishie
Malawi
No comments:
Post a Comment