Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano
katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini
mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria. (Picha
na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Dkt. Stergomena Tax akila kiapo mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano
katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini
mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria. (Picha
na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuteuliwa na kula kiapo kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC umemalizika leo
tarehe 20 Agosti 2017 katika mji wa Pretoria Afrika Kusini ambapo Wakuu
wa nchi na Serikali wa SADC kwa kauli moja wamempongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake katika Asasi
ya Ushirikiano wa siasa , Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli, kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha uongozi wake
akiwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo.
Tanzania imemaliza kipindi chake cha
Uenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama
tarehe 19 Agosti, 2017 wakati wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa nchi wanachama wa SADC ambao umefanyikia hapa Pretoria,
Afrika Kusini kuanzia tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.
Akizungumzia mambo muhimu yaliyojadiliwa
katika mkutano huo wa 37 wa SADC, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amemuwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema pamoja
na mambo mengine SADC imetambua na kuthamini mchango wa Tanzania katika
kipindi cha Uongozi wa Asasi ya Saisa , Ulinzi na Usalama iliyokuwa
chini ya Rais Dkt. John Pombe magufuli.
Amesema Tanzania imeshakuwa Mwenyekiti
wa Asasi hiyo mara tatu, kwa nyakati tofauti ambapo mara ya kwanza
ilikuwa ni kipindi cha 2006/2007 na mara ya pili ilikuwa ni 2012/2013 na
mara ya tatu katika kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017 chini ya
uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli, ambapo alikabidhiwa kijiti cha uongozi huo kutoka kwa Jamhuri
ya Msumbiji wakati wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali
uliofanyika Falme ya Swaziland tarehe 30 Agosti, 2016.
Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana
wakati wa Uenyekiti wa Tanzania katika Asasi hiyo ni kusimamia uchaguzi
wa Bungenchini Seychelles ambao ulifanyika mwezi Septemba, 2016.
Aidha katika kipindi cha Uongozi wa
Tanzania ulisaidia kurejesha hali ya amani na utulivu nchini Lesotho
ambayo kwa muda mrefu tangu 2014 imekuwa kwenye mgogoro wa kisiasa
pamoja na kushughulikia matatizo ya Uchaguzi nchini DR Congo.
Mkutano wa 37 wa SADC pia umemuongezea
muda mwingine Mtanzania Dkt. Stergomena Taxi kuendelea na wadhifa
aliokuwa nao wa Katibu Mtendaji wa SADC kwa kipindi cha miaka minne
mingine ambapo atatumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2021.
Dkt. Tax amethibitishwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliomaliza leo na kuapishwa rasmi kushika nafasi hiyo.
Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na
Serikali (SADC) umehitimishwa kwa kutolewa Tamko (Communique) kuelezea
yaliyojiri katika Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali ikiwa ni pamoja na
mkutano wa 38 kufanyika nchini Namibia.
Imetolewa na ;
Ofisi ya Makamu wa Rais
Pretoria, Afrika Kusini
20 Agosti, 2017.
No comments:
Post a Comment