Sunday, August 13, 2017

TIMU YA WATAALAM MANISPAA YA UBUNGO NA OFISI YA MKUU WA MKOA DSM WATEMBELEA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUKAGUA MAENEO YANAYOTARAJIWA KUJENGWA OFISI ZA UTAWALA

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Timu ya wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo ikiongozwa na Afisa Elimu msingi Bi Chausiku Masegenya kwa kushirikiana na timu ya wataalam kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikiongozwa an Afisa Elimu Mkoa Ndg.Hamisi Lisu leo Jumapili ya tarehe 13/08/2017 imetembelea shule zote zilizochaguliwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Utawala mara baada ya kikao cha pamoja leo saa mbili na nusu asubuhi  katika ukumbi wa manispaa Kibamba.

Akizungumza katika kikao kabla ya kuanza ziara Afisa Elimu Mkoa aliomba ofisi ya Mkurugenzi iandae godown kwa ajili ya kupokelea vifaa vya ujenzi wa ofisi zote vitakavyotolewa na Mh.Paul Makonda kabla ya kutawanywa kwenye mashule kwa ajili ya ujenzi huo.

Ziara hii imetokana na agizo la mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda kwa kila Manispaa kuhakikisha kuwa shule zilizochaguliwa zina eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hizo.

Ikumbukwe kuwa Mh. Mkuu wa Mkoa amejitolea kujenga majengo ya ofisi za utawala 100 ndani ya mkoa wa Dar es alaam na Ubungo kama Manispaa mojawapo ilipata mgao wa majengo 18. Katika mgao huo Manispaa iliamua majengo 6 yawe ya sekondari na 12 yawepo kwenye shule za msingi.

Shule za sekondari zilizochaguliwa kwa ajili ya kujengewa ofisi hizo ni Kibwegere, Kwembe, Mbezi inn, Goba, King'ongo na Urafiki. Kwa upande wa shule za Msingi ni Kwembe, King'anzi, Kisopwa, Msakuzi, Malamba Mawili, Kibesa, Kulangwa, Tegeta A, Kunguru, Urafiki, Kawawa na Msumi.

Katika ziara hiyo shule zote zilikuwa na eneo la ujenzi wa ofisi hizo. Vile vile hata maeneo kwa ajili ya utendaji vifaa na malazi ya mafundi yalikuwepo. Kwa zile shule ambazo hazikuwa na maeneo ya kutunza vifaa na malazi ya mafundi. Bodi na kamati za shule waliahidi kutoa baadhi ya madarasa au ofisi pasipo kuingilia masomo au utendaji kazi kwa namna yoyote ile.

Afisa Elimu Msingi aliwashukuru wajumbe wa Bodi na Kamati za shule kwa Ushirikiano mzuri walioutoa na kuwaomba kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mafundi watakaokuja kuweka kambi kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hizo.

MWISHO

No comments:

Post a Comment