Msaidizi Meneja Uhusiano wa Benki
ya Exim Ernest Typa akiwakaribisha wageni waalikwa katika maadhimisho ya
miaka 20 ya Benki hiyo yaliyofanyika katika Tawi lake liliopo mtaa wa
Mlandege Mjini Zanzibar. (kulia) Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Fedha Shirika
la Taifa la Biashara Zanzibar Ismail Omar Bai.
Baadhi ya wateja wa Exim Bank
walioshiriki maadhimisho ya miaka 20 ya Benki hiyo wakifuatilia sherehe
hizo zilizofanyika katika Tawi lao mtaa wa Mlandege Mjini Zanzibar.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya
miaka 20 ya Exim Bank Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Taifa la
Biashara Zanzibar Ismail Omar Bai akikata keki ya miaka 20 ya benki hiyo
katika sherehe zilizofanyika Tawini kwao Mlandege Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga Znz.
Na Khadija Khamis – Maelezo 15/08/2017.
Mkurugenzi wa Fedha Shirika la
Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Ismail Omar Bai amewataka
wafanyabiashara na wateja wa Exim Bank kuekeza amana zao katika benki
hiyo.
Akizungumza katika maadhimisho ya
sherehe za kutimiza miaka 20 ya Exim Bank yaliyofanyika katika Tawi lao
lililopo Mlandege Zanzibar, alisema iwapo wafanyabiashara na wateja
wataendelea kuwekeza maendeleo ya Exim Bank yatafikiwa kwa haraka .
Alisema katika kipindi cha miaka
20 tokea kuanzishwa Exim Benk imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilling
za kitanzania TirionI 1.5 ikiwa ni makusanyo ya amana za wateja .
Aidha aliishauri Exim Bank
kuimarisha huduma kwa wateja wao ili kuwavutia wananchi wengi zaidi
kuweka amana zao na kuwa moja ya benki zenye kuleta ushindani wa
kibiashara Tanzania .
Nae Meneja Mkuu wa Tawi la hilo
Frederick Robert Umiro ametoa shukrani kwa wafanya biashara pamoja na
wateja kwa kuwaunga mkono na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara .
Alisema Exim Bank inatowa mikopo
kwa wanachama wake ikiwemo mikopo ya wafanyabiashara wadogo wadogo na
wakubwa ambao huweza kukopeshwa kwa riba ya asilimia 18.
Akizungumzia mikopo ambayo huwapa
wateja wao ni yamikopo mikubwa ya ujenzi wa nyumba usafirishaji bidhaa
kilimo utalii na mengineo kwa lengo la kuweza kujikwamua na umasikini
Alisema Exim Bank ilianza mwaka
1997 ikiwa na tawi moja la Samora mjini Dar es salaam na hivi sasa
imeweza kuengeza matawi yake kufikia 33 kwa Tanzania jambo ambalo ni
maendeleo makubwa kwa Benki hiyo.
Alifahamisha kuwa katika kutanua
huduma zake wamefanikiwa kufungua matawi matano Uganda, matano
Visiwa vya Comorro na matawi matatu nchini Djibout.
Nae mmoja wa wateja wa Exim Bank
Bi Asma Makame ameipongeza Benki hiyo kwa kuwajali wateja wao na
kuwataka kuiengeza huduma ili iwe kivutio kwa wananchi wengi kujiunga .
Akieleza changamoto
wanazokabiiliana nazo ni ushindani wa kibiashara na mabenki mengine
ambayo kila moja hutumia mbinu za kuvuvutia wateja kwa kutumia mbinu
mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa unafuu katika baadhi ya huduma zao .
No comments:
Post a Comment