Tuesday, August 15, 2017

UVCCM YAWATAKA VIJANA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Vijana wa CCM wilayani Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba katika ukumbi wa mkutano Tawi la CCM Wawi. (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)
Maafisa wadhamini,wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani wakimsikilizaKaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) wakati akizungumza na maafisa wadhamini wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani,katika ukumbi wa skuli ya Chekechea Mdungu wilayani Chake Chake Mkoa wa Kusini pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) (kulia) akizungumza na viongozi wa kikundi cha Vijana wa Jasiriamali  wa mboga mboga (Mtaji wa masikini) wadi ya Pujini mara maada ya kukagua mazao mbali mbali yanayolimwa na kikundi hicho.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua mradi wa kikundi cha Vijana wa Jasiriamali  wa mboga mboga (Mtaji wa masikini) Wadi ya pujini
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  wakati akizungumza na maafisa wadhamini,wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani, katika ukumbi wa skuli ya chekechea mdungu wilayani Chake Chake Mkoa wa Kusini pemba.
Maafisa wadhamini,wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani wakimsikiliza ndg: Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  wakati akizungumza na maafisa wadhamini,wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani,katika ukumbi wa skuli ya chekechea mdungu wilayani Chake Chake Mkoa wa Kusini pemba.

Na Mathias Canal, Kusini-Pemba

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umewataka vijana  kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili kuepusha wimbi la ukosefu wa ajira nchini na kuacha tabia ya kushiriki katika  vitendo viovu ambavyo  vinahatarisha usalama wa Taifa.

Akizungumza na Maafisa wadhamini wa wizara, Madiwani, Wakurugenzi wa mabaraza ya Mji wa Chakechake na Mji wa Mkoani,  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ni sehemu sahihi kwa vijana ambapo pia inawasaidia kuondoka na vitendo vya matumizi ya dawa ya kulevya.

Alisema kuwa kiasi kikubwa cha fedha za mikopo hutolewa kila mwaka na Wakurugenzi wa Mji kwa ajili ya vijana ambapo  upande wa kundi la vijana wanapatiwa asilimia tano na wanawake asilimia tano kati ya asilimia 10 iliyotengwa.

Shaka alisema kuwa  wakurugenzi wanapaswa kusimamia vyema utoaji huo wa fedha  kwani lengo la kutolewa fedha hizo ni kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi ili kujiendeleza kimaisha .

Sambamba na hayo pia Shaka amewasihi madiwani kutokuwa watu wa kulalamika na badala yake kuwaonyesha vijana mbinu bora ya mafanikio na fursa zilizopo katika Halmashauri.

Alisema kuwa wanapaswa kuendelea kumsaidia Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohamed Shen sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

Aidha, Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka ametembelea na kuwasalimu wagonjwa ikiwemo kuwapatia baadhi ya vifaa tiba sambamba na baadhi ya mahitaji katika Hospitali ya Wilaya ya Chakechake.

MWISHO

No comments:

Post a Comment