Kaimu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.
Na Mathias Canal, Pemba
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka amehitimisha ziara ya siku
nne ya kikazi Kisiwani Pemba-Zanzibar kwa kuzuru katika Mikoa yote miwili
ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba na Wilaya zake zote za Wete, Mkoani,
Chakechake na Micheweni.
Katika
ziara hiyo pamoja na mambo mengi alikagua na kushiriki kufanya kazi za kijamii
ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020,
kushiriki kuona shughuli mbali mbali za uzalishaji Mali kupitia makundi ya
vijana na kuwasaidia kwa kuwaunga mkono ili kuongeza mtaji wa
miradi yao.
Alitumia
ziara hiyo kuzungumza na makundi ya vijana kwa nyakati tofauti, viongozi
wa CCM, jumuiya za CCM Pamoja na kushiriki shughuli zingine mbalimbali za
kijamii, kiuchumi na kisiasa na kuwaasa kukaa maskani pekee pasina kufanya kazi
za uzalishaji mali jambo ambalo litapeleka mbele maendeleo katika jamii.
Katika
maeneo yote aliyozuru Kaimu Katibu Mkuu huyo alitilia zaidi msisitizo kwa
vijana kujiunga na vikundi mbalimbali vya kijamii ili kupatiwa mikopo ya vijana
inayotolewa na serikali kwa asilimia 5 kila mwezi.
SALAMU
KWA MALIM SEIF
Katika
hatua nyingine Shaka alimtumia salaamu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF
aliyesimamishwa uongozi Maalim Seif Shariff Hamad kwa kumtaka kuacha
kueneza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao kwani kuhubiri siasa za
mgawanyiko ni utaratibu wa kiongozi asiyekuwa mweledi kwani maendeleo
hayahitaji ubaguzi dhidi ya wananchi.
"Juhudi
za SMZ na SMT katika kuwatumikia wananchi hazitadumazwa kwa maneno ya wapinzani
badala yake zitaendeleza mikakati yake ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm
ya mwaka" Alisema Shaka
Alisema
ni Siasa uchwara kuhubiri mgawanyiko katika jamii na kutumia nasaba na asili
ili kusaka madaraka, kiongozi ambaye atajiegemeza katika siasa chafu milele
hawezi kupata ridhaa ya wananchi.
"Nimeshiriki
ujenzi wa shina hili nikiwa na furaha kwenye mtima wangu, Msisahau kumpelekea
salamu Maalim Seif Shariff Hamad mwambieni asichoke kueneza siasa za mgawanyiko
CCM na serikali zake haizitaacha kabisa kuwapelekea maendeleo wananchi bila
kuwabagua" Alisema Shaka
Shaka
alisema kuwa Kiongozi au mwanasiasa anayekusudia kupata imani na amana ya
wananchi hawezi kushiriki kuwagawa watu bali huwa kiranja wa kuwaunganisha na
kuwataka wawe wamoja huku wakiishi kwa maelewano na mshikamano.
Alisema
kuwa Wakati dunia, vyama vya siasa makini, wanaharakati na mashirika ya
kimataifa yakihubiri uwepo wa amani, maelewano na kukataa mgawanyiko,
itashangaza kumsikia mtu anayejiita kiongozi akihubiri siasa chafu za mgaanyiko
na mifarakano.
"Tunamsubiri
tena Seif Sharif Hamad mwaka 2020 tumpige mara ya saba, sijui atawania Urais
kwa CUF ipi, ile ya Profesa Lipumba haimtaki, yake yeye haitambuliwi na Msajili
wala hana Bodi ya Wadhamini, akija tutamgaragaza ili aje kupumzika Mtambwe
" Alisema Shaka
Ziara
ya Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka imeacha
gumzo kubwa kwa wananchi kufunguka kiakili na kumualika tena kwa mara nyingine
kwani tayari wamewelewa namna wanavyopotoshwa na viongozi wa vyama vya
upinzani.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment