Thursday, August 17, 2017

REAL MADRID YAIDUNGUA 2-0 BARCELONA NA KUCHUKUA UBINGWA WA SPANISH SUPER CUP

DHYwJddXsAA6kq6
Real Madrid wameendeleza ubabe kwa mahasimu wao wakubwa Barcelona kwa kuwapa kipigo cha pili, safari hii ikiwa ni mabao 2-0 na kufanikiwa kubeba ubingwa wa Spanish Super Cup.
 
Madrid iliitwanga Barcelona kwa mabao 3-1 nyumbani kwao Camp Nou, Barcelona.
 
Bila ya mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo aliyelambwa kadi nyekundu katika mechi ya kwanza, Madrid imeshinda kwa idadi hiyo ikiwa nyumbani Santiago Bernabeu.
1502919289296_lc_galleryImage_MADRID_SPAIN_AUGUST_16_Ma
Marco Asensio alikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya nne tu ya mchezo na Karim Benzema akapachika la pili dakika ya 39 baada ya kumuibia mpira beki Samuel Umtiti wa Barcelona.
1911
Madrid imechukua ubingwa ikiwa na jumla ya mabao 5-1 baada ya ushindi wa mabao 3-1 ugenini Camp Nou.

No comments:

Post a Comment