Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii
Bw. Patrick Golwike akihamasisha wananchi kuendeleza ari ya kushiriki
kazi za maendeleo ya kijiji chao cha Ufyemba mkoani Iringa kwa
kushirikiujenzia wa zahanati hiyo ambayo unajengwa na wananchi wa
kijiji hicho kwa kutumia nguvu za wananchi wenyewe ili kusogeza huduma
za afaya kijijini.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinda
akishirikiana na wakazi wa Kijiji cha Ufyambe kubeba matofali katika
kufanikisha ujenzi wa Zahanati kijiji cha Ufyemba kata ay wasa, iliyoko
wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.
Wananchi wa kijiji cha Ufyambe
wakishiriki katika kubeba matofali na kujenga jingo la zahanati ya
kijiji hicho ili kuondokana na taatizo la kutembea umbali mrefu kutafuta
huduma za afya.
Wananchi wa kijiji cha Ufyambe
wakimsikilizakwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati
akiwahamasisha kujitolea katika kuibua, kupanga na kutekeleza shughuli
za maendeleo katika Kijiji chao.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi
mifuko 50 ya saruji kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyemba Bw Ronaganius
Lunyungu ili kuunga mkono jitihada za wananchi hao katika kukamilisha
ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ufyemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi
pesa kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyambe Bw Roganius Lunyungu
zilizopatikana katika harambee ili isaidie katika kumalizia Ujenzi wa
zahanati ya kijiji cha Ufyambe.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga
akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ufyambe kata ya Wasa wilaya ya
Iringa vijijini mkoa wa Iringa katika jitihda za kuhamasisha ujenzi wa
zahanati ya kijiji hicho.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha
Ufyambe wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(hayupo pichani)
alipofanya ziara ya kushiki kwa vitendo kazi za miradi ya maendeleo
iliyoibuliwa na kutekelezwa kwa kutumia nguvu za wananachi wenyewe
katika kijiji hicho.
Picha na Erasto Chin’goro WAMJW IRINGA
……………………………………………………………….
Na Erasto Chin’goro WAMJW
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Bibi Sihaba Nkinga
amewahamasisha wananchi kujitolea katika kutekeleza shughuliza maendeleo
ikiwa ni sehemu ya kuhamsha ari wananchi kufanya kazi za maendeleo yao.
Ameyasema hayo katika ziara yake
Mkoani Iringa wakati katika jitihada zake za kuhakakisha jamii inahuisha
ari ya kushiriki shughuli za kujitolea na uanzishaji wa miradi
inayoibuliwa na kutekelezwa na wananachi wenyewe kwa kushiriki kazi
mbalimbali za utekelezaji wa shughuli hizo katika maeneo ya mijini na
vijijini.
“Dhana ya maendeleo ya jamii
inawataka wananachi kujitolea kushiriki kazi za maendeleo kwa
kushirikisha kubaini mahitaji na changamoto zinazowakabaili wananachi na
kujadiliana pamoja kuhusu mbinu za utatauzi wa changamoto hizo” alisema
Bibi Sihaba.
Bibi Sihaba ameongeza kuwa
wananchi waendelee kuainisha ushiriki wao katika kukamilisha miradi hiyo
ya pamoja kwa kutumia rasilimali na nguzu kazi ya ndani badala ya
kutegemea misaada ya nje ya jamii.
Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wananchi katika
maeneo mengine kuiga mfano bora wa kijiji cha Ufyambe ili kujiletea
maendeleo bila kusubiria msaada wa Serikali kuu.
Dhana hii ya kujitolea katika
kutekeleza shughuli za maendeleo imefanikisha kijiji cha Ufyambe kata
ya Wasa kilichoko wilaya ya Iringa vijijini, mkoani Iringa kushirikiana
na wananchi kukamilisha ujenzi wa zahanati ili kupata uhakika wa huduma
za afya kwa watoto, wanawake, na jamii kwa ujumla.
Katika tukio hili, Katibu Mkuu
aliongozana na uongozi wa mkoa wa Iringa ukiongozwa na KAtibu tawala
Mkoa wa Iringa Bibi Wamoja Ayoub, viongozi wa wilaya ya Iringa vijijini,
uongozi wa kata ya Wasa na kijiji cha Ufyambe.
No comments:
Post a Comment