Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack
Kengese akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
kuhamasisha shughuli za kilimo na elimu kwa wananchi.
Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na
Ushirika katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Godwin Everygist
akifafanua jambo kwa wananchi wakati wa uhamasishaji wa shughuli za
kilimo.
Ofisa Elimu Sekondari halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Cleophas akihamasisha wananchi kushiriki shughuli za elimu.
Ofisa Elimu Msingi halmashauri ya
wilaya ya Kishapu, Moshi Balele akizungumza wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya uhamasishaji elimu na kilimo kwa wananchi.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi wilayani Kishapu.
Na Mwandishi Maalumu, Kishapu
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu
mkoani Shinyanga imezindua kampeni kabambe ya kuhamasisha wananchi
kushiriki katika shughuli za kilimo na elimu.
Imezindua kampeni hiyo katika
kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi ambayo itashirikisha wananchi katika
vijiji vyote vya wilaya hiyo ili kuinua hali za wananchi kiuchumi na
kielimu.
Akizindua kampeni hiyo wa niaba ya
Mkuu wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba, Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack
Kengese alisema kila mwananchi ana wajibu wa kutumia fursa ya ardhi
kujiletea maendeleo.
Kengese alimiza wananchi kulima
mazao yanayostahimili hali ya ukame kutokana na hali ya hewa ya wilaya
hiyo ambayo hupata mvua chini ya wastani unaotakiwa.
Alisema halmashauri ya wilaya hiyo
kwa kutambua hali ya hewa ilitunga sheria ndogo mwaka 2008 ya kilimo
cha mazao yanayostahimili ukame na hifadhi ya chakula cha kutosha kwa
kaya.
“Sheria hii imemtaka kila mkazi wa
wilaya ya Kishapu kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwa ni pamoja na
kuhifadhi chakula cha kutosheleza mahitaji ya familia angalau miaka
miwili au zaidi.
“Aidha sheria hii ilitungwa ili
kutuhakikishia usalama wa chakula muda wote hivyo ni rai yangu kuwa
wananchi wote tutashiriki katika shughuli za kilimo kwa kulima mazao
yanayostahimili ukame,” alisisitiza.
Aidha, Kengese aliongeza kuwa
sheria imetaja adhabu kwa mtu atakayekadi adhabu yake ni kifungo
kisichozi miezi 12 au kulipa faini isiyozidi sh. laki tatu au adhabu
zote mbili.
Pia aliwataka maofisa kilimo
waisimamie sheria hiyo kikamilifu na kuwa yeyote atakayekaidi afikishwe
kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment