Rais Muhammadu Buhari na makamu wake Yemi Osinbajo katika uwanja wa ndege wa Abuja, 19 08 2017.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, jana Jumamosi amerejea nyumbani
akitokea London Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu kwa takribani
miezi mitatu.
Buhari amepokelewa na Wafuasi wake
waliojipanga katika barabara za mji mkuu wakiimba na kucheza, ambapo
maafisa wa ngazi za juu serikalini akiwemo makamu wake nao walikusanyika
kumkaribisha Buhari.
Buhari mwenye umri wa miaka 74 aliondoka
nchini mwake mnamo Mei 7 ambapo kutokurejea kwake kwa muda mrefu
kulisababisha mvutano ambapo wananchi waliandamana na kutoa wito kumtaka
arejee nyumbani au ajiuzulu.
Taarifa ya ikulu imeeleza kuwa rais Buhari, atalihutubia taifa Kesho Jumatatu.
Chanzo:RFI
No comments:
Post a Comment