Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw.
James Ihunyo (wapili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyokopeshwa na
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wilayani
humo. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya
Kilimo.
Makamu Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula, Bw. Mohamed Dadi (kushoto) akionesha maendeleo ya Skimu hiyo wakati
Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia) pamoja na Kaimu
Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi
kutoka wilayani na Benki ya Kilimo walipotembelea Skimu hiyo.
Kaimu
Afisa Tarafa ya Mang’ula, Bw. Omary Said (kulia) akitoa maelezo kuhusu
Mradi wa Kilimo Shadidi kinachofanyika katika Kijiji
cha Msolwa Ujamaa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kushoto) na
Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati).
Wengine wanaosikiliza na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya
Kilimo.
Meneja
Ufuatiliaji na Tathamini ya Mikopo wa TADB, Bw. Dickson Pangamwawe
(wapili kushoto) akionesha maendeleo ya ukuaji wa miwa ya
Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa ambao ni wanufaika wa mikopo
ya Benki ya Kilimo. Wanaotazama ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Mkuu wa Wilaya
ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege.
Wakulima wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa wakipanda mpunga kwa kutumia njia ya kilimo shadidi.
Maafisa
kutoka Benki ya Kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero
wakingalia Mpunga uliyo tayari kuvunwa katika Skimu ya Umwagiliaji
ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa.
Katika
kuhakikisha miradi inayopatiwa mikopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB), uongozi wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Mkuu wa
Wilaya ya Kilombero,
Bw. James Ihunyo wametembelea miradi minne iliyopo wilayani humo.
Miradi iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS, Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula. Nyingine ni
Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga alisema ameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo hali
inayochochea ari
ya Benki katika kutimiza lengo la Serikali la kukopesha wakulima
nchini.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo
aliwaasa wakulima hao kurudisha mikopo kwa wakati ili wakulima wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo.
“Lengo
la mikopo hiyo ni kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini
Tanzania, hivyo kuchelewesha mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma
juhudi
hizi,” Bw. Ihunyo alisema.
Zaidi ya Shilingi bilioni 2 imekopeshwa kwa wakulima wa mpunga na miwa wilayani Kilombero.
No comments:
Post a Comment