Na Lucas Raphael, Igunga
MWALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Igurubi, Maganga Ngassa (35)
amefi kishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya kufanya
mapenzi na mwanafunzi wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari kidato
cha nne, Kata ya Mwisi wilayani hapa.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi Igunga, Elimajid Kweyamba alidai mbele
ya Hakimu Juhudi Mdonya, kwamba Julai 25, mwaka huu saa 9 alasiri katika
nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Forest au Chacha
iliyoko Mtaa wa Mwayunge mjini Igunga, kinyume na sheria za nchi, Ngassa
alifanya mapenzi na mwanafunzi wa mwenye umri wa miaka 17 anayesoma
shule ya sekondari iliyoko Kata ya Mwisi kidato cha nne (jina
linahifadhiwa). Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo
imeahirishwa hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment