Chuma Suleiman
maarufu kama Bi Hindu amesema hana shida na mabadiliko katika klabu ya
Simba, lakini atazungumza hadi hapo atakapopata kilichotokea kwenye
mkutano maalum wa wanachama wa Simba uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam na kupitisha mfumo mpya wa uendeshaji.
Wanachama zaidi ya 1200 wa Simba wamekubali klabu yao kuendeshwa kwa mfumo wa hisa huku mmoja pekee akipinga.
Bi Hindu amesema hakuhudhuria mkutano huo kwa kuwa alikuwa katika harakati za kumuozesha mjukuu wake.
“Nilikuwa busy na
harusi ya mjukuu wangu na sasa akili yangu ni mechi ya Yanga. Kuhusiana
na hilo la mabadiliko sawa tu, nakubaliana. Lakini nitazungumza lolote
hadi nitakaposikia kile kilichotokea.
“Kwa sasa nitazungumza nini, sijui waliamua kumpa Mo, au wameamua vingine. Sasa sijui hasa kilichofanyika hapo,” alisema.
Bi Hindu amekuwa kati ya wale waliokuwa wakipinga kufanyika kwa mkutano huo ambao uliitwa mkutano maalum wa wanachama wa Simba.
No comments:
Post a Comment