Tuesday, August 8, 2017

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA (NANE NANE) KITAIFA MWAKA 2017


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla wakati wa kufunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.(Picha zote na Mathias Canal)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kushoto) akijadili jambo na Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Lindi Mhe Salma Kikwete wakati alipotembelea Mabanda ya Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew Mtigumwe akiwasalimu wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla wakati wa sherehe za Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu Teknolojia ya Serikali ya Mtandao Kutoka kwa Bi Caroline Munuo Marealle Mtaalamu wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati alipotembelea banda la wizar ahiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akizungumza kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kuhusu utuzwaji wa bata mzinga kwenye banda la JKT wakati wa kufunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akihimiza jambo alipokuwa akizungumza kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango kwa zawadi mbalimbali wakati alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kabla ya kufunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akihimiza jambo alipokuwa akizungumza kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Shamba Darasa la JKT kabla ya kufunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt Hussein Mansoor kuhusu kilimo cha mazao mbalimbali mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kabla ya kufunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Baadhi ya Wananchi Kutoka Mkoa wa Lindi na Mtwara wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.



Na Mathias Canal, Lindi


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8 Agosti 2017 amefunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi.

Akizungumza wakati akiwahutubia wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla Makamu wa Rais amesema kuwa serikali inahakikisha kuwa kila Mtanzania ananufaika na fursa mbalimbali za uchumi zilizopo nchini, Kwa kutambua kuwa zaidi ya asilimia 65.5 ya watanzania wanajihusisha ama wameajiriwa na kujiajiri katika sekta za Kilimo, Ufugaji na uvuvi.

Alisema kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali na  za makusudi za kuimarisha sekta hizo za Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa kuzifuta na kuzipunguza baadhi ya Kodi, Tozo na Ada ambazo zimekuwa kero kwa wakulima na wananchi.

Alisema kuwa pamoja na kuzifuta na kuzipunguza Kodi, Tozo na Ada lakini pia serikali imechukua hatua za makusudi za kupunguza ushuru wa mazao uliokuwa unatozwa na Serikali za Mitaa kutoka asilimia 5 hadi asilimia 3 kwa mazao ya biashara na asilimia 2 kwa mazao ya chakula.

Mhe Suluhu alitilia msisitizo kuwa kuanzia sasa ni marufuku kwa mtu yeyote kutoza ushuru kwa mazao yanayosafirishwa kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine, ambayo uzito wake hauzidi tani moja kwani ushuru wa mazao unatozwa kwenye Halmashauri ambako mazao hayo yanatokea na siyo kila yanakopita.

Hatua nyingine iliyochukuliwa ni ya kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vyakula vya mifugo vinavyotengenezwa hapa nchini ili kupunguza gharama ya kununua chakula hicho kwa wafugaji.

Aidha, alisema kuwa Serikali pia imesamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye mayai ya kutotoleshea vifaranga, lengo likiwa ni kupunguza gharama ya uzalishaji vifaranga na kukuza Sekta ndogo ya Ufugaji ili iweze kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan alisema kuwa serikali itaendelea kuboresha na kuendeleza misingi mahususi ili kuongeza kasi ya kuleta mapinduzi makubwa katika kilimo, mifugo na uvuvi.

Alisema kuwa kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane inayosema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati” inaunga mkono juhudi za Serikali za kufikia uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.

Awali Mhe Samia akisoma salamu za Mhe. Rais wa Jamhurri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alisema kuwa Mhe Rais anawapongeza wananchi kwa kuendelea kumuunga mkono kwenye jitahada za mapambano dhidi Rushwa, kurudisha nidhamu kwa watumishi wa umma na kujenga Tanzania mpya yenye kuendeshwa na uchumi wa viwanda huku akiwaomba wananchi kuendelea kulipa kodi kwa wakati na kudai risiti kila wanunuapo bidhaa.

Alisema kuwa Mhe Rais Magufuli yupo bega kwa bega na wananchi na ataendelea kupunguza utitiri wa kodi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi. 

MWISHO.

No comments:

Post a Comment