Tuesday, August 8, 2017

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATEMBELEA BANDA LA UBUNGO NANENANE MOROGORO

NA Mwandishi Wetu, Morogoro

Ikiwa leo ni kilele cha wiki ya nanenane banda la Manispaa ya Ubungo limebahatika kutembelewa na Mheshimiwa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Mhe. Makonda aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam  Teresia Mbando.

Akiwa katika banda hilo Mhe. Makonda amepata fursa ya kujionea vipando mbalimbali ikawajee ni pamoja na migomba iliyopandwa kwa ustadi mkubwa.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amejionea teknolojia ya usafishaji wa maji, mtambo wa kutengeneza umeme, bwana la kufugia samaki, kilimo mjini, kitalu nyumba, mifugo mbalimbali na wafanyabiashara wanaofanya usindikaji wa vyakula kutokana na mazao wanayolima.

Mkuu wa mkoa amepokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ambae amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ujio wake katika banda la Ubungo ambayo ni Manispaa yenye umri wa  miezi 11 tu lakini wamefanya vizuri katika maonesho haya kwa kushiriki na kuwepo kwa mambo ya kuvutia katika banda hilo

Pia Mkuu wa mkoa mara baada ya kuzungukia banda hilo nakupata maelezo hakusita kutoa pongezi kwa Mkurugenzi Mkurugenzi kwa ushiriki wenye tija licha ya uchanga katika maonyesho hayo.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment