Na Judith Mhina – MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, anahitaji
kupata usaidizi wa kutosha kutoka kwa viongozi na hasa wasaidizi
kuanzia ngazi ya nyumba kumi hadi taifa.
Maneno
hayo yametamkwa na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
alipofanya mahojiano na Idara ya Habari – MAELEZO - ofisini kwake
Oysterbay Jijini Dar-es-Salaam.
Jaji
Warioba ameona kuna udhaifu mkubwa wa kiutendaji ambapo wananchi
hawatoi changamoto zinazowakabili mpaka wamuone Rais amefika katika eneo
lao, au wanaeleza changamoto zinazowakabili kwa viongozi husika ila,
viongozi hawazifanyii kazi, ambapo wananchi wanaamua kuziwasilisha kwa
Rais mara wanapomuona.
“Rais
hawezi kufanya kazi peke yake naomba tuimarishe utendaji wetu wa kazi,
kama utendaji ungekuwa mzuri suala la makontena kufika hadi bandarini
lisingekuwepo, na hata kugundulika kwake kusingefanywa na Rais,” amesema Jaji Warioba.
“Nampongeza
sana Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia
Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kwa utendaji wao wa
kazi. Viongozi hawa ni wasikivu na wanatekeleza kazi zao bila mihemko
kwa kutoa maagizo na maelekezo kwa wahusika ili wayatekeleze”, aliongeza Mhe. Warioba.
No comments:
Post a Comment