Leo hii Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeshiriki katika uzinduzi wa maonesho ya nanenane yanayofanyika leo kikanda katika Mkoa wa Morogoro viwanja vya Nanenane Mwalimu Julius Nyerere,ambapo Mgeni Rasmi ni Waziri Maliasili na Utalii Mh.Profesa.Jumanne Maghembe.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ni miongoni mwa Halmashauri mpya iliyofanikiwa kushiriki maonesho haya licha ya upya wake tayari ina eneo lake kama Halmashauri katika viwanja hivyo ambapo katika kipindi kifupi tayari kuna vipando vya aina mbalimbali,bwawa la samaki,mabanda ya kisasa ya ufugaji wa n'gombe,mbuzi,kuku,bata bila kusahau green house iliyoshamiri vipando n.k.
Akiongea katika maonesho hayo mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob amesema uamuzi wa serikali kuleta maonesho haya umesaidia katika uboreshaji wa kilimo na inawapa fursa wajasiriamali kujulikana na kujitangaza kisha kuinua uchumi,pia wananchi kupata elimu ya kilimo kwa ujumla wake.Pia amewataka wananchi kuendelea kuja kujionea mambo tofauti na mazuri yaliyofanywa kwa kipindi kifupi katika banda la Ubungo.Amewataka wananchi wajiyokeze kwa wiki yote hii ya maadhimisho mpaka siku ya kilele ambayo ni tarehe 8/8/2017.
Nae Kaimu Mkurugenzi Ally J Ally akizungumza mara baada ya uzinduzi amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kujionea mambo mazuri yaliyoko katika banda la Halmashauri ya Manispaa ya ubungo.
Katika banda hilo la Manispaa wananchi wamepata fursa ya kujionea wataalamu mbalimbali na kupewa elimu juu ya utengenezaji na usindikaji wa vyakula,ufugaji kwa ujumla wake,mbinu za kisayansi katika kusafisha maji yenye tope na kuwa safi na salama kwa kunywa,ufugaji wa samaki wa kisasa ambapo wamejionea bwawa linalotumika kufugia samaki hao mubashara likiwa na samaki,pia sehemu za machinjio ya kisasa na kadharika.
Baadhi ya wananchi waliohojiwa wamesema wanapongeza Halmashauri hii kwa utendaji uliotukuka kwani mambo wanayoyaona kwenye banda hili hayafanani na muda mfupi wa Manispaa hii toka ianzishwe,kwani mambo mazuri yamefanyika katika kipindi kifupi hii inadhihirisha utendaji mzuri wa kazi chini ya Uongozi wa Mkurugenzi John L.Kayombo.
Maonesho haya ya Kikanda yameshirikisha mikoa ya Tanga,Dar es salaam,Morogoro,Pwani.Kauli mbiu ya maonesho haya kwa mwaka huu ni"ZALISHA KWA TIJA MAZAO NA BIDHAA ZA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI ILI KUFIKIA UCHUMI WA KATI.
HONGERA WAKULIMA
HONGERA MANISPAA YA UBUNGO
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO UMC
No comments:
Post a Comment