Katika kituo cha kupigia kura cha Gatundu, nchini Kenya.
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Kenya imesema kuwa matokeo
itakayoyatangaza yatakuwa ni kwa mujibu wa sheria na sio kwa maelekezo
ya mtu au kundi fulani la wanasiasa.
Kauli ya IEBC imekuja ikiwa ni saa
chache tu zimepita toka muungano wa upinzani nchinuij Kenya, NASA
utangaze matokeo yake iliyosema yametokana na uhakiki walioufanya
kupitia kwenye fomu zilizowekwa kwa kanzi data ya IEBC inayotumiwa
kujumusha matokeo.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati
amekiri kupokea barua ya muungano wa NASA ambapo amesema tayari
wameshawarudishia majibu ambayo nao wamesisitiza kuwa matokeo waliyo
nayo sio rasmi.
IEBC inasisitiza kuwa matokeo
yatakayotangazwa hayatatokana na karatasi peke yake lakini yatatokana na
idadi ya wapiga kura waliojitokeza na kupiga kura kuchagua kiongozi
wanaemtaka.
Chebukati amewataka wanasiasa kujiepusha na kufanya kazi za tume yake ambayo ndio yenye mamlaka ya mwisho kumtangaza mshindi.
Tume imejibu barua hii na matokeo sahihi
na yakisheria yatatangazwa baada ya tume kupokea fomu zote za matokeo
namba 34 B, kwa mantiki hiyo tume itatangaza matokeo ya urais kama
inavyoelekezwa na ibara ya 138-3C na ile ya 138-10 ya katiba”
Awali mmoja wa vinara wa muungano wa
NASA Musalia Mudavadi wakati akizungumza na wanahabari jijini Nairobi,
alieleza kuwa muungano wao umefanya uhakiki wa fomu zilizoko kwenye
kanzi data ya IEBC na kujiridhisha kuwa mgombea wao Raila Odinga ndie
mshindi.
Mudavadi alienda mbali zaidi na hata
kuitaka tume ya uchaguzi kutotangaza matokeo ambayo yatakuwa kinyume na
yale ambayo wamethibitisha kupitia kwenye mtandao wao.
Mpaka sasa ukweli haujajulikana kuhusu
nani ameibuka mshindi kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga ambapo
kwa mujibu wa tume ya uchaguzi IEBC, matokeo rasmi huenda yakatangazwa
leo mchana baada ya kukamilisha uhakiki wa fomu namba 34 A na B kutoka
kwa maafisa wa uchaguzi.
Shughuli nyingi zimeendelea kusimama
jijini Nairobi na kwenye maeneo mengine ya nchi, ambapo wafanyakazi
wachache wa uma walifika ofisini huku maelfu wakishindwa kutokana na
hofu ya kutokea vurugu.
Siku ya Alhamisi waangalizi wa kimataifa
wa uchaguzi pia walitoa taarifa zao za awali ambapo wengi walieleza
kuridhishwa na namna tume ya uchaguzi IEBC iliandaa uchaguzi ambao
wamesema kwa kiwango kikubwa ulikuwa Huru na Haki.
Chanzo:RFI
No comments:
Post a Comment