Na Is-haka Omar, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi Zanzibar kwa
moyo mkunjufu kinapongeza na kuisifu kitendo kilichofanywa na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuongeza pencheni kwa Wastaafu
waliomaliza utumishi wao wakipokea mshahara wa kima cha chini
serikalini.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo
vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya
Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Bi. Waride Bakari Jabu amesema ongezeko
la shilingi 50,000 ni sawa na asilimia 125 lililofanywa na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, linajibu masuala mengi ya msingi ya kiuchumi,
kisiasa na kijamii.
Akielezea kufarajika kwake na
kiwango hicho cha pencheni kilichoongezwa kwa wastaafu, Katibu huyo wa
Kamati Maalum ya NEC Zanzibar amesema suala la kuongeza shilingi 50,000
hadi kufikia shilingi 90,000 kinatakiwa kupongezwa na wananchi.
Amesema kitendo hicho
kilikofikiwa na Serikali (SMZ) cha kuamua kuwaongezea wastaafu wake
pensheni kinalenga sio tu kuwasaidia wastaafu hao kupambana na hali
ngumu ya maisha, bali pia kwa kiasi kikubwa kitaleta uwiyano wa karibu
na nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi wa Serikali liyofanyika hivi
karibuni.
Ameeleza kuwa CCM pia
inaipongeza serikali ya awamu ya saba kwa imeimarisha maslahi ya
watumishi wa umma katika kuongeza viwango vya mishahara ya kima cha
chini kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 300,000 ambalo ni ongezeko
la asilimia 100, pamoja na kutekeleza mpango wa utoaji wa pencheni
jamii kwa wazee wote waliofikisha miaka 70 bila ya kujali kazi aliyokuwa
akiifanya.
Hata hivyo, Bi. Waride ameiomba
Serikali kupitia Wizara yenye Mamlaka ya Fedha kufanya kila
linalowezekana kuhakikisha wastaafu waliokuwa na nyadhifa serikalini
wanapatiwa pensheni kulingana na nyadhifa walizokuwa nazo hapo kabla.
Aidha amesema CCM inaridhishwa
na kasi ya Dkt. Shein katika Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka
2015/2020, hivyo tunawasihi wananchi na viongozi wa Serikali kufuata
nyayo hizo kwa kumsadia kiongozi huyo ili Taifa lizidi kuimarika
kiuchumi.
No comments:
Post a Comment