Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka(wa kwanza kushoto) akishiriki ujenzi wa Jengo la maskani Mtambwe Wilayani wete.
wanachama wakimlaki Kaimu katibu mkuu mara baada ya kuwasili kuzungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Wete wakifuatilia kwa Umakini mkutano huo.
Kaimu katibu wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha (UVCCM) ndg:Dorice Obed akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khadija Nassoro Ally akizungumza katika Mkutano wa ndani akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba
Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Umeipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi Visiwani Pemba.
UVCCM imesema kuwa RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amefanya
mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ikiwemo kuundwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya
ndege vya Zanzibar jambo ambalo litaongeza mapato kwa serikali na vipato kwa
wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka
Hamdu Shaka leo Agosti 17, 2017 alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa
Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini
ya muundo wa Umoja wa Kitaifa (SKU) imepata mafanikio makubwa katika kipindi
cha uongozi wa miaka saba cha Dkt Shein.
Alisema kuwa kuwepo kwa Serikali hiyo kumeweza
kuleta maelewano ya kisiasa pamoja na
kuvishirikisha vyama vingine katika uwezeshaji wa serikali.
Alisema kuwa sekta ya elimu imeimarika kwa kiasi
kikubwa jambo ambalo linazidi kurahisisha upatikanaji wa elimu bora ikiwemo
kuimarika kwa mishahara ya wafanyakazi Visiwani Zanzibar.
Alisema kuwa uvumilivu wa kisiasa
na kuheshimu Katiba na sheria ndio siri ya mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar ikiwemo kuheshimu katiba, utawala bora, kupinga udhalilishaji kwa
watoto na wanawake.
Shaka yupo ziarani Kisiwani Pemba ambapo atatembelea mikoa yote miwili ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba ambapo pia atazuru katika Wilaya zote nne ikiwa ni pamoja na Wilaya ya Wete, Micheweni, Mkoani na Chakechake kwa kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment