Na Mahmoud Ahmad Arusha
Waziri wa maliasili na utalii Jumanne Maghembe amewataka wananchi wanaoishi pori tengefu la loliondo kuondoka katika pori hilo ili kupisha shughuli za uhifadhi.
Aliyasema hayo katika Hafla ya kuwatunuku vyeti wamiliki wa hotel zinazokidhi viwango vya ubora vya kuwalaza wageni.
Amesema kuwa, Zipo
hekari elfu mbili zilizotengwa na serikali kwa ajili ya wananchi ambazo
zimeshaelekezwa huduma muhimu lakini wananchi hawataki kukaa kule.
Maghembe amesema
kuwa, wananchi wamekuwa wakidanganywa na taasisi zisizo za kiserikali
kuendelea kuishi katika maeneo ya pori tengefu la loliondo ambapo jambo
hilo ni kinyume cha sheria ya uhifadhi wakati serikali ilishatenga
hekari elfu mbili na mia tano kwa ajili yao.
Akasisitiza kwamba
huduma muhimu za kijamii zimeshazogezwa katika eneo hilo ambapo hadi
sasa wananchi wamekuwa wakisita kuhamia katika maeneo hayo na kuendeleza
maisha yao jambo ambalo serikali inawataka kuhakikisha wanahamia katika
maeneo ambayo serikali imewatengea.
Aidha aliongeza kuwa
,Rais Magufuli alishasema Watu wenye mifugo mingi waiondoe kwenye
hifadhi ama wapunguze mifugo ili wabaki na michache ya kujikimu.
No comments:
Post a Comment