Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw.
James Ihunyo (wapili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa
miradi iliyokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
wilayani humo. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw.
Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na
Benki ya Kilimo.
Makamu Mwenyekiti wa Skimu ya
Umwagiliaji ya Mkula, Bw. Mohamed Dadi (kushoto) akionesha maendeleo ya
Skimu hiyo wakati Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili
kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga
(katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo
walipotembelea Skimu hiyo.
Kaimu Afisa Tarafa ya Mang’ula,
Bw. Omary Said (kulia) akitoa maelezo kuhusu Mradi wa Kilimo Shadidi
kinachofanyika katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa kwa Mkuu wa Wilaya ya
Kilombero Bw. James Ihunyo (kushoto) na Umoja wa Wakulima wa Miwa wa
Msolwa Ujamaa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga
(katikati). Wengine wanaosikiliza na viongozi waandamizi kutoka wilayani
na Benki ya Kilimo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima
wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege (kushoto) akiongea na
ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ulioambatana na Mkuu wa Wilaya
ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kulia). Benki ya Kilimo ilifanya ya
ukaguzi wa miradi iliyopatiwa mikopo ili kujionea maendeleo ya miradi
wilayani Kilombero.
Meneja Ufuatiliaji na Tathamini
ya Mikopo wa TADB, Bw. Dickson Pangamwawe (wapili kushoto) akionesha
maendeleo ya ukuaji wa miwa ya Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa
Ujamaa ambao ni wanufaika wa mikopo ya Benki ya Kilimo. Wanaotazama ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia). Kushoto ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian
Sanindege.
Maafisa kutoka Benki ya Kilimo na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakingalia Mpunga uliyo tayari
kuvunwa katika Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa.
IMG_1813
Wakulima wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa wakipanda mpunga kwa kutumia njia ya kilimo shadidi.
Katika kuhakikisha miradi inayopatiwa
mikopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), uongozi wa Benki
hiyo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw. James Ihunyo wametembelea miradi minne iliyopo wilayani humo.
Miradi iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS,
Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula. Nyingine ni Umoja wa Wakulima wa Miwa wa
Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema ameridhishwa na
maendeleo ya miradi hiyo hali inayochochea ari ya Benki katika kutimiza
lengo la Serikali la kukopesha wakulima nchini.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo aliwaasa wakulima hao kurudisha mikopo kwa wakati ili wakulima wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo.
“Lengo la mikopo hiyo ni kuinua ukuaji wa
uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, hivyo kuchelewesha mikopo
hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma juhudi hizi,” Bw. Ihunyo alisema.
Zaidi ya Shilingi bilioni 2 imekopeshwa kwa wakulima wa mpunga na miwa wilayani Kilombero.
No comments:
Post a Comment