Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides
(TGGA), Anna Abdallah (katikati) akiwa na Girl Guides waliorejea nchini
kutoka kwenye programu ya Yess ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya
uongozi, utamaduni na maadili katika nchi za Uganda, Madagascar,
Zimbabwe na Zambia. Hapo ilikuwa wakati wa hafla maalumu iliyoandaliwa
na TGGA Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapongeza na kupata mrejesho wa
walichojifunza walipokuwa kwenye programu hiyo inayodhaminiwa na
Norwey.Anna Abdallah aliwapongeza wasichana hao wanne kwa kuiwakilisha
vizuri TGGA na Tanzania katika programu hiyo nje ya nchi.
Kutoka kulia ni Ummy Mwabondo alikwenda Zambia, Farida Mjoge aliyekuwa Uganda, Elizabeth Betha (Madagascar) na Edna Chembele (Zimbabwe),
Girl Guides hao wakipata msosi wakati wahafla ya chakula cha usiku
iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Oysterbay,
Dar es Salaam.
Anna Abdallah akiotoa nasaha na pongezi kwa Girl Guides kwa
kuiwakilisha vizuri TGGA NA Tganzania kwa ujumla, ambapo aliwataka
watumie mafunzo waliyoyapata kwa kutoa mafunzo kwa wasichana wenzao
nchini.
Wakiwa na furahani Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kushoto), Anna Abdallah (katikati) na Mjumbe wa TGGA, Agnes Makenya
Katibu Mkuu wa TGGA Tanzania, Grace Shaba akitoa neno la ukaribisho
muda mfupi kabla ya Girl Guides waliorejea nchini kutoka nje ya nchi
kwenye programu hiyo kuelezea mambo mbalimbali waliyoyafanya na
kujifunza
Grace Shaba akiwatambulisha Girl Guides hao
i Ummy Mwabondo akielezea kwa njia ya picha kazi mbalimbali alizokuwa anazifanya alipokuwa Zambia
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia
Mjema akitoa ufafanuzi wakati Girl Guides wakielezea mafanikio na
changamoto ya mafunzo yao nje ya nchi
Girl Guides Farida akielezea mambo mbalimbali aliyoyafanya akiwa Uganda kwa muda wa miezi sita.
No comments:
Post a Comment