WILAYA YA KIGOMA MJINI
- Amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa mashina na matawi wapya waliochaguliwa, kata na wilaya ya Kigoma mjini wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika ukumbi wa mikutano Kizito Kigoma mjini.
- Ametembelea na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, kikundi cha vijana wanaojishuhulisha mradi wa uwekezaji viwanda vidogo vidogo utengeezaji sabuni na usimikaji wa dagaa katika kata ya Mwanga
- Amezungumza na wanachama wa CCM na jumuiya zake, wazee waasisi, wakinamama na vijana ofisi ya kata ya Gungu na kisha kushiriki ujenzi wa Taifa wa ofisi ya kata hiyo ambalo lilijengwa mwaka 1962-1963 na sasa linafanyikwa ukarabati mkubwa.
- Hadi kukamilika kazi ya ujenzi wa ofisi hiyo ya kata jumla ya T. Shs 2,094,500 zinahitajika ambapo Kaimu katibu Mkuu amendesha harambee ya papo kwa papo na jumla ya T. shs 355,000/= taslim zilikusanywa na vifaa vyenye thamani ya T.shs 1,160,000/= vilichangwa ili kukamilisha ujenzi huo.
-Ametembelea eneo la uwekezaji la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kigoma ambalo taratibu zimekamilika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha uwekezaji cha biashara.
*WILAYA YA KIGOMA VIJIJINI.*
-Pamoja na viongozi aliofatana nao wameshiriki katika ufyatuaji wa matufali katika kikundi cha Mgera Youth Group katika kata ya Mwandinga cha wajasiriamali wanaojishuhulisha na shuhuli mbali mbali za uzalishaji zinazofanywa ikiwemo kufyatua tufali za kuchoma, kutengeneza sabuni, uvuvi na mradi wa visa kilichoanzishwa mwaka 2015.
-Mbunge wa viti maalum Vijana Mkoa wa Kigoma Zainab Katimba amewachangia wanakikundi hao vyarahani 5 na Kaimu Katibu Mkuu amewachangia Fedha taslim kuchangia mfuko wao wa hisa cha kuweka na kukopa cha vijana hao.
-Amezindua shina la wakereketwa na kisha kuzungumza na vijana kundi kubwa la vijana katika kata ya Kagongo kijiji cha Mgaraza ambapo pia aliwapokea viongozi 19 waandamizi wa wilaya na kata toka katika vyama vya upizani vya CUF, ACT wazalendo na NCCR Mageuzi ambao aliwakaribisha na kuwakabidhi kadi za CCM.
-Ametembelea na kushiriki kazi ya uchimbaji msingi kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika kijiji cha Kalinza na Mlagala ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM 2015/2020 mradi ambao utagharimu T.shs 786,642,000/= Fedha zinazotoka katika Mfumo Mkuu wa Serikali.
-Wakati huo amekabidhi kadi kwa wanachama wa CCM na jumuiya zake waliotimiza masharti ya uanachama kikatiba na kikanuni kama ifuatavyo:-
CCM 591
UVCCM 482
UWT 82 na
WAZAZI 62
Ziara ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) itaendelea kesho katika wilaya ya Buhingwe na Kasulu.
No comments:
Post a Comment