Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula leo amefanya mkutano wa hadhara eneo la Shule ya Msingi Bugugumuki Ibanda Kata ya Kirumba Kuhamasisha Maendeleo, kusikiliza Kero za Wananchi na kuzipatia Ufumbuzi akiambatana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga, Madiwani na wataalamu wa Manispaa ya Ilemela
Akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo waliojitokeza kuelezea Kero na Changamoto mbalimbali zinazowakabili Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kuelezea shughuli mbalimbali za kimaendeleo zilizotekelezwa na zinazoendelea kutekelezwa tangu Serikali ya awamu ya Tano chini Rais Mhe Dkt John Magufuli iingie madarakani amewataka Wananchi hao kuunga mkono shughuli zinazotekelezwa na Serikali ikiwemo Zoezi la Ulipaji Kodi, Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo na Urasimishaji Makazi ambapo amesema
‘…Baada ya Urasimishaji zoezi linalofuata ni umilikishwaji, Usipopata Hati yako suala la Urasimishaji kwako ni kazi bure utajua tu mipaka lakini huwezi kufaidika na ardhi yako, Hakikisheni mnapatiwa Hati ili uweze kuitumia kwa shughuli nyengine hata kama unapata mwekezaji hawezi kuja kwenye eneo lisilokuwa na hati unapopata Hati unaongeza thamani ya eneo lako, Unapopata Hati una uhakika wa kumiliki, Unapopata Hati unakuwa na uhakika wa mipaka …’
Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kusisitiza juu ya Ushirikiano na kuhamasisha wananchi wake kujitoa kwa hali na mali katika kujiletea maendeleo amewataka wananchi hao kuzingatia sheria ya ulipaji wa kodi ya upangishwaji nyumba ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima kwa kulipa kodi hiyo kwakuwa kodi hiyo ipo kwa mujibu wa sheria
Akimkaribisha Mbunge huyo Diwani wa Kata ya Kirumba Mhe Alex Ngussa amempongeza Mbunge huyo kwa ushirikiano na usimamizi mzuri wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotekelezwa katika Kata yake na Jimbo la Ilemela kwa ujumla huku wataalamu kutoka Shirika la Umeme nchini Tanesco Mkoa wa Mwanza chini ya Muhandisi Lucas Mtabilu na Mhandisi Stan William kutoka Mwauwasa wakiwaelezea wananchi hao juu ya miradi mbalimbali wanayoitekeleza katika jimbo hilo kama jitihada ya kuzipatia ufumbuzi kero zinawakabili wananchi wa Ilemela
Wakati huo huo Mbunge Mhe Dkt Angeline Mabula leo amehudhuria Uzinduzi wa Zoezi la Kampeni ya Umezeshaji wa Dawa za Kukinga na Kutibu Ugonjwa wa Kichocho na Minyoo ya Tumbo lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela katika Viwanja vya Shule ya Msingi Isenga
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
18.07.2017
No comments:
Post a Comment