Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,(Utumishi na Utawala bora)Mh.Anjela Kairuki ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kasi nzuri katika zoezi la uhakiki linaloendelea la kuoanisha taarifa za watumishi na zile zilizopo NIDA.
Waziri huyo ametoa pongezi hizo leo 18/7/2017 katika ukumbi wa chuo cha sheria mawasiliano ambapo amekutana na watumishi wa Manispaa ya Ubungo ikiwa ni siku yake ya pili katika manispaa hiyo akisikiliza kero mbalimbali za watumishi.
Mhe Kairuki amesema kwamba Halmashauri hiyo mpaka sasa imefikia asilimia 80.6 ikiwa ni tofauti na Manispaa zingine hivyo kuifanya Ubungo kuongoza kwa wilaya zote za Dar es salam.
Akiongea katika mkutano huo ameelezea pia kutangazwa kwa ajira 10,184 ili kuziba pengo la walioondolewa katika utumishi baada ya uhakiki,na si hivyo tu bali kutakuwa na ajira zingine 52,400 hivi karibuni.
Aidha akizungumzia suala la ulipwaji wa mishahara ya mwezi amesema kwa sasa mishahara ya watumishi kuanzia sasa italipwa kwa pamoja na hakutakuwa tena na utofauti wa tarehe za kupokea mshahara kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Ametoa msisitizo katika masuala kadhaa yafuatayo:
*Nidhamu kazini
*Uchapa kazi kwa bidii
*Watumishi kujituma
kufuatilia taarifa zao
na kujiunga na mtandao wa portal ambao ni maalum kwa ajili ya kuhifadhi taarifa zao za kikazi.
* kutofanya kazi kwa mazoea
*Kufuatilia taratibu za kitumishi ili kujua haki zao.
*Umuhimu wa kujiendeleza kielimu kwa watumishi.
Akijibu kuhusu upandaji wa madaraja na stahiki zao ameaema serikali imetenga pesa kwa ajili ya kulipa malimbikizo na wote walistahili kupanda watapandishwa ndani ya mwaka huu.
Mwisho alishukuru Uongozi wa Manispaa kwa ushirikiano mzuri na mapokezi mazuri katika ziara yake ya siku 2.
Tumenufaika na ziara ya Mh.Waziri tunasema asante na karibu tena Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
No comments:
Post a Comment