- Amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa mashina na matawi wapya waliochaguliwa wa chama na jumuiya zake kutoka katika kata zote za wilaya Uvinza.
-Ametembelea na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, Jengo jipya la wakinamama na sehemu ya jengo la upasuaji katika kituo cha afya Nguruka ambapo pia alikabidhi msaada wa vifaa tiba mbali mbali pamoja na kutoa sabuni kwa wagonjwa waliolazwa wodi ya watoto na akinamama wajawazito.
-Wakati huo huo vijana wa CCM waliendesha harambee ya kuchangia mashuka 40, shuka 20 zimechangiwa na mbunge wa viti maalum Mhe Zainab Katimba alichangia shuka 20, katibu hamasa UVCCM wilaya ya Uvinza alishangia shuka 20, viti 20 na meza 3 zilichangiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Nguruka kwa ajili kituo hiko cha afya.
-Amekabidhi msaada ya machine mbili za kufyatulia matufali kwa vikundi vya vijana toka kata mbili za nguruka na nyangabo kisha kuzungumza na vijana hao.
-Ametembelea na kufanya mazungumzo na vijana waliojikusanya kufanya shuhuli za ujasiriamali ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito wa Mhe Rais Magufuli kwa vijana kujituma na kufanya kazi ili kuinua kipato chao.
-Amekabidhi kadi mpya za CCM na kupokea wanachama wapya waliohama 82 toka vyama vya CUF, ACT wazalendo na NCCR Mageuzi katika kata ya Nguruka.
-Ametembelea mradi wa vijana wa kuuza mbegu na pembejeo za kilimo.
-Amezungumza na vijana, wanakimama na wazee wa CCM katika kata ya Kazuramimba ambapo jumla ya vijana 226 kutoka CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na ACT wazalendo wamerudisha kadi na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.
-Wakati huo amekabidhi kadi kwa wanachama wa CCM na UVCCM walitimiza masharti ya uanachama kikatiba na kikanuni.
Jioni leo Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) amewasili wilaya ya Kigoma Mjini kuendelea na Ziara jumanne 18/07/2017 katika wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment