Jana tarehe 16/07/2017 Ndg Humphrey polepole katibu wa Halmashauri kuu Taifa,Itikadi na Uenezi alifanya ziara ya ndani ya kichama katika Wilaya ya Temeke Dar es salaam, kata ya miburani, mbagala kuu na mbagala.
Katika ziara hiyo ndugu Polepole aliambatana na Katibu wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndg Kusilawe, wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa na wajumbe wote wa kamati ya siasa ya wilaya Wakiongozwa na Katibu wao CCM wa Wilaya
Ziara hiyo ya ndugu polepole lengo lake lilikuwa ni kusikiliza na kutatua Changamoto mbalimbali za wanachama wa Msingi wa CCM ngazi ya shina, matawi na kata akigusia maeneo ya miradi, uchaguzi na undeshaji wa chama.
Kata ya miburani, ndugu polepole amesisitiza pamoja na mambo mengine wanachama waombe nafasi za uongozi katika maeneo wanayoishi/makazi yao na isitokee mwanachama wa eneo lingine kuomba nafasi ya uongozi eneo ambalo siyo mkazi.
Kata ya Mbagala Kuu, licha ya kupokea changamoto lukuki ndugu polepole aliagiza kamati ya siasa wilaya ya temeke kuwasimamisha uongozi wote wa kata ya mbagala kuu kwa sababu ya kushindwa kusimamia, kuendesha na kuuhisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata hiyo.
Pia Kata ya mbagala ndugu polepole ametoa onyo kali kwa wanachama ambao wanaendeleza makundi ya uchaguzi wa mwaka 2015 hadi leo, jambo ambalo linadhoofisha umoja wa wanachama wa CCM
Kwa upande Mwingine ndg Mwenezi Amemuagiza Katibu wa CCM MKOA Dar ES SALAMA kupeleka Wakaguzi wa Mapato na Matumizi ya Kata ya Miburani na Mbagala Kuu baada ya kuonekans kuna Uvujaji wa mali za Chama na Mikataba mibovu ya Mali za Chama.
Mwisho: Polepole amesisitiza CCM Mpya itajengwa na wanachama wa msingi na wangazi zote kwa viongozi kutenda haki na wanachama kutimiza wajibu wao.
" Haki ya wanachama lazima ibaki haki ya wanachama haki haibagui mwanachama yoyote" Alisema ndugu Polepole.
No comments:
Post a Comment