Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, leo tarehe 18/7/2017 amefungua mafunzo ya mgambo kwa vijana wa wilaya ya Kigamboni.
DC Mgandilwa amewahasa vijana hao kuwa wavumilivu katika kipindi chote cha mafunzo ili wavishwe uzalendo kwa ajili ya kuitumikia nchi yetu na kusisitiza kuwa vijana ambao wamepitia mafunzo ya Mgambo watakuwa wakipewa kipaumbele pale zitakapojitokeza nafasi za kwenda JKT.
Aidha, DC Mgandilwa amewatahadharisha vijana hao kutojihusisha na vitendo vya kihalifu baada ya kupata mafunzo hayo yanayojumuisha matumizi ya siraha.
Pia amesema Ofisi yake itaandaa utaratibu mzuri wa kualika na kushirikisha makampuni ya ulinzi yaliyopo Kigamboni ili siku ya kufunga mafunzo waje na kuajili watu watakaooona wanafaa ambao hawataajiliwa serikalini.
Mafunzo hayo yamekusanya jumla ya vijana 109 kutoka katika kata 9 za wilaya ya Kigamboni.
No comments:
Post a Comment