Saturday, July 15, 2017

UVCCM SHINYANGA MJINI YAMUUNGA MKONO MH.RAISI KWA KAZI NZURI ANAZOZIFANYA KWA KUCHANGIA DAMU KATIKA KITUO CHA AFYA KAMBARAGE

NA COMRADE EGOBANO

Umoja wa vijana wa ccm jana Tarehe *14/7/2017* wamejitokeza kwa wingi vijana zaidi ya sabini katika kituo cha Afya Kambarage  na kuchangia damu zaidi ya uniti 37 , kitu ambacho kilipongezwa saana na wananchi na wakazi wa Wilaya ya Shinyanga mjini hususani wanaoishi eneo la kata ya Kambarage.

Pamoja na Shughuli hiyo pia walijitolea kufanya usafi wa eneo lote la kituo cha Afya cha Kambarage lengo likiwa ni kumuunga mkono Mh.Rais kwa kazi nzuri anayoifanya pia kwa kumkabidhi gari la Kubebea Wagonjwa *Ambulance*

Mh.Mbunge viti maalumu kutoka katika wilaya yetu, alisema Kijana mmoja sisi kama vijana hatuna sababu ya kutomuunga mkono Mh.Rais kwa hiki alichotufanyia katika wilaya yetu, pia katibu uvccm wilaya ya Shinyanga Mjini alipata pongezi kutoka kwa Mh.Mbunge vitu Maalumu Dada *Lucy mahenga* kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuhamasisha vijana kuchangia damu, na akamuomba isiishie leo tu, iwe ni utaratibu wa kila baada ya miezi mitatu.

No comments:

Post a Comment