Saturday, July 15, 2017

Ndg HUMPHREY POLEPOLE ASHIRIKI MAOMBI YA KULIOMBEA TAIFA -UWANJA WA UHURU DSM

Ndugu Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole amehudhuria na kushiriki Maombi ya kuliombea Taifa leo jijin DAR ES SALAMA TANZANIA katika Uwanja wa Uhuru na Waumini wa Kristo pamoja na Wanasiasa Mbali Mbali na Viongozi wa SerikalI

Lengo la Mkusanyiko huo wa Madhebu Mbali Mbali Nchini ni Kuliombea Taifa,Viongozi pamoja na Mh Rais na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kulitumikia Taifa letu.

Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole wakati wanapomkea kuwasili kwake hapo Uwanjani amewapongeza Sana Wachungaji, Maaskofu na Wakristo wote Waliokusanyika kuliombea Taifa Lao Pendwa mama Tanzania

Ndugu Humphrey Polepole Amesema hakuna kitu Muhimu na Chenye Thamani kubwa Duniani kote kama Amani, Upendo na Mshikamano hasa kwa TAIFA lenye kubwa kama Tanzania.

Nao Viongozi Mbali Mbali wadini, Wachungaji na Maaskofu  
Wamejitokeza kwa wingi na hamasa kubwa yenye Upendo Mkubwa sana kwa Taifa na Serikali nzima inayongozwa na Mh Rais Dr. John Pombe MAGUFULI Kiongozi.Kiongozi Wetu Mzalendo kweli Kweli

Lakini pia Waumini wamejitokeza kwa Wingi kuliombea Taifa lao ili liendelee kuwa na Amani, Mshikamano, Nchi pia Salama na kufanikisha Malengo ya kuwalekeza Maendeleo Watanzania 

AHSANTE SANA

No comments:

Post a Comment