Kwa niaba ya Watumishi wote wa Manispaa ya Ubungo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg. JOHN LIPESI KAYOMBO anatoa shukrani za dhati kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe ANGELA KAIRUKI kwa kitendo chake cha kuja kutembelea Manispaa ya Ubungo (ziara ya siku mbili) sambamba na kusikiliza na kutatua matatizo mbalimbali ya Watumishi hao.
Shukrani hizo zinaakisi Mhe Waziri kusikiliza matatizo yote ya Watumishi kwa usawa bila upendeleo wa aina yoyote pia kwa kujibu maswali kwa ufasaha na upendo uliokithiri.
Kwa kushirikiana na jopo la wataalamu alioongozana nao walifafanua na kuwafundisha Watumishi mambo mengi ambayo awali walikuwa hawayafahamu.
Watumishi wa Manispaa ya Ubungo wamefurahishwa na ukarimu wa Mhe Kairuki sambamba na utendaji wake wa kazi.
"Watumishi wa Manispaa ya Ubungo wanashukuru sana kwa kuja kuwatembelea sambamba na kusikiliza na kutatua kero zao pia kuwafundisha mambo mengi ambayo awali walikuwa hawayafahamu, nashukuru sana kwa ujio wako Mhe. Waziri Angela Kairuki" alisema Mkurugenzi Kayombo na kuendelea :
"Ulikubali kusikiliza kila mtumishi aliyetaka kuuliza swali ama kuzungumza chochote bila kujali njaa wala muda wa kuondoka, ubarikiwe sana" alisema Mkurugenzi Kayombo.
Mwisho Mkurugenzi Kayombo amewataka Watumishi wa Manispaa ya Ubungo kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano yenye kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu"
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
No comments:
Post a Comment