Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibondo Salome akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka wakati wa kusain kitabu cha Mahudhurio ya wageni wilayani kibondo.
KAIMU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka (wa pili kulia), akiwa katika mradi wa ufugaji samaki kwenye Kijiji cha Ming'inya wilayani Kibondo mkao wa Kigoma, juzi. Kuhoto ni Mbunge wa Viti Malumu, Zainb Katimba (CCM). Picha zote na Fahadi Siraji-UVCCM)
Mhe Mbunge wa Viti Maalum Vijana Zainab Katimba akitoa mchango wa fedha katika kikundi cha kinamama katika kijiji cha minyinya wilaya ya kibondo mkoani kigoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka akishiriki Kulima katika shamba la kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka akishiriki upandaji mbogamboga katika shamba shamba la kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka wa pili kulia akizungumza na kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka akikagua kikundi cha Ujasilia mali cha mafundi wenyeulemavu katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.
Mbunge wa Viti Malumu, Zainabu Katimba (Kulia) akishiriki Kulima katika shamba la kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
..........................................................................................................
KAIMU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka (wa pili kulia), akiwa katika mradi wa ufugaji samaki kwenye Kijiji cha Ming'inya wilayani Kibondo mkao wa Kigoma, juzi. Kuhoto ni Mbunge wa Viti Malumu, Zainb Katimba (CCM). Picha zote na Fahadi Siraji-UVCCM)
Mhe Mbunge wa Viti Maalum Vijana Zainab Katimba akitoa mchango wa fedha katika kikundi cha kinamama katika kijiji cha minyinya wilaya ya kibondo mkoani kigoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka akishiriki Kulima katika shamba la kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka wa pili kulia akizungumza na kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka akikagua kikundi cha Ujasilia mali cha mafundi wenyeulemavu katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.
Mbunge wa Viti Malumu, Zainabu Katimba (Kulia) akishiriki Kulima katika shamba la kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
..........................................................................................................
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Umoja wa Viijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM ) umesema
vijana wanaoendelea kulalamika bila kufanya kazi, kujituma na kutoa
jasho la uchapakazi watakawia sana kufikia malengo chanya na kujikwamua
hatimaye maisha.
Hayo yameelezwa jana kaimu katibu mkuu shaka Hamdu Shaka
alipotembelea kikundi cha ujasiriamali katika kata ya Mwandiga wilaya ya
Kigoma vijijini Mkoani hapa .
Shaka alisema hakuna njia mbadala na ya mkato ya kujikwamua
kimaisha na hali ngumu yoyote ya umasikini bila kijana mwenyewe kuamua
kujishughulisha na kuzalisha mali hatimaye kujitegemea.
Aliwasifu wana kikundi hicho kwa kujikusanya, kupanga
mipango na mikakati ya mradi wa kufyatua matofali, kuzalisha sabuni na
kuwa na kikundi cha Vicoba kwa mtimdo wa kuweka na kukopa pia kununu
hisa.
"Vijana wengi huwa wanawaza, wanapanga na kutaka kutenda
hawatendi, kikundi hiki ni makini na kimeamua kuonyesha kwa vitendo
jinsi kilivyopania kujikwamua na umasikini wa vipato hatimaye kujijenga
kiuchumi "Alisema Shaka .
Shaka aliwahimiza watendaji wa halmashauri ya Kigoma
vijijini kuona haja ya kukipa umuhimu kikundi hicho kwa kuwapatia
wataalam, mitaji na vyanzo vya fedha.
"Vijana mnakawia, jiungeni ili kushiriki katika shughuli za
ujasiriamli kwa lengo la kuacha utegemezi badala yake mjiajiri na
kujitegemea kiuchumi kama kikundi cha "Alisema
Kaimu Katibu Mkuu pia alizindua kazi za uchimbaji wa mitaro
kwa akili ya usambazaji wa maji safi na salama katika kata ya kalinzi
na kutazama maendeleo ya mradi wa ujenzi wa tangi la maji hatimaye
akazumgumza na wanachama katika kikao cha ndani katika kata Mgaraganza
mkoani hapa .
Kwa upande wake Mbunge wa vijana Mkoa Kigoma Zainab Katimba
ameahidi kukisaidia kikundi hicho kwa kuwapatia vyerehani vitano ili
kuongeza mradi mwingine wa ushonaji kwa kina dada wa kikundi hicho.
Aliwaeleza vijana hao waendelee na shime hiyo ya kujitolea
na kutumia nguvu zao ili kufikia malengo yao ya kujijenga kiuchumi na
kupata maisha bora.
"Ingelikuwa vijana wote kigoma na Tanzania wanapitisha
maamuzi mazito kama kikundi hiki, nchi yetu isingekuwa na vijana
wanaolalamika, wanaosaka ajira au kulalamikia umasikini "Alisema
Zainab.
Hata hivyo Mbunge huyo alisema atafanya kila linalowezekana
kuhakikisha vijana hao halmshauri ya Kigoma vijijini inawafuatilia na
kuwatazama kwa macho mawili makoni vijana hao.
End
No comments:
Post a Comment