Friday, July 21, 2017

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MOHAMED JUMANNE MTATURU MKONONGO

Kumbukumbu ya Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo

Kuzaliwa 11/03/1973 - Kufariki 21/07/2016

Zimepita saa, siku, miezi na hatimaye leo mwaka mmoja umetimia tangu ututoke ghafla kunako Alhamisi, tarehe 21 Julai  2016.

Tunakukumbuka kwa upendo, ucheshi, ukarimu na moyo wako wa kusaidia wahitaji. Tumejifunza mengi kutokana na maisha yako na tutaendelea kukuenzi kwa yale mema na mazuri uliyotenda hapa duniani.

Unakumbukwa sana na mama yako mzazi Amina Mtaturu, mke wako mpenzi Naiz Mavura, watoto wako wapendwa Nassa na mdogo wake Nolan-Idrissa; kaka na dada zako, wakwe zako, shemeji zako pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zako lukuki.

Tunamshukuru Mungu ambaye anaendelea kutupa nguvu ya kuishi pasi na uwepo wako--ni mmoja wa neema na miujiza yake Allah. Tunaendelea kukuombea dua ili Mungu aendelee kukupumzisha kwa amani huku ukitusubiri katika Ufalme wake wa milele.

Inna Lillah wa Inna Illayh Raj'un--
"Sisi ni wa Mwenyezi mungu na kwake Tutarejea"

No comments:

Post a Comment