Friday, July 21, 2017

NAIBU MKUU WA CHUO TAALUMA DUCE ATEMBELEA IDARA YA ELIMU SEKONDARI MANISPAA YA UBUNGO

Naibu Mkuu wa chuo Taaluma chuo Kikuu kishiriki cha elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa Godliving Mtui leo amefanya ziara Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kutembelea idara ya elimu sekondari.

Ziara hiyo iliyokuwa na malengo ya kujitambulisha, kupata taarifa fupi juu ya mwenendo wa elimu sambamba na kujua maeneo ya shule za sekondari katika Manispaa ya Ubungo, kujadili zoezi la wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya mafunzo kwa vitendo (teaching practice) katika shule mbalimbali za sekondari  zilizopo katika Manispaa hiyo ilihusisha mazungumzo kati ya Naibu Mkuu huyo na Kaimu Afisa elimu sekondari wa Manispaa hiyo Ndg. Neema Maghembe.

IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

No comments:

Post a Comment