" Asubuhi baada kusikia kilio cha Vijana wanaojituma wakilalamika kukosa mikopo toka Halmashauri hasa 5% za Vijana na wanawake" Shaka
"Mwenyekiti wa Halmashauri nilikutaka utoe ufafanuzi umeniongopea mimi najua na nina taarifa za ndani Fedha hizo hazitoki kama ilivyoagizwa katika ilani" - Shaka
"Ninao ushahidi 2016/2017 kuna ubabaishaji mkubwa vikundi mlivyotoa havizidi kimoja" - Shaka
"Kuna urasimu mkubwa maafisa wahusika wanatoa mikopo kama ni 2,000,000/anakata laki tano mtu anachukua chake cha juu watendaji hao wanatuhumiwa majina yao ninayo Mhe DC" - Shaka
"Mnategemea Fedha hiyo wakishaichukua vijana watakwenda kuwekeza vipi na waweze kurejesha marejesho kwa wakati alafu mnalalamika eti vijana hawarudishi Fedha" - Shaka
"Tunaposema tunamunga mkono Rais Magufuli tumuunge kwa vitendo ukweli, uadilifu na uzalendo" - Shaka
"Nikiwa miongoni mwa wasimamizi wa ilani ya CCM nakuomba DC upo hapa jambo hili lirekebishwe mara moja nikiondoka vyenginevyo litafika mbali na vijana sisi tutalala na mtu mbele" Shaka
"UVCCM tumeamua kufuatilia kwa karibu changamoto za vijana wenzetu na tumekusudia kuirudisha jumuiya yetu waliko vijana kwa kuguswa na shida na changamoto zao" - Shaka
"UVCCM tumeamua kuwa kiunganishi na mdomo wa vijana katika mambo muhimu na nyeti kwalengo la kumsaidia Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli" - Shaka
No comments:
Post a Comment