Saturday, July 22, 2017

SHAKA ABISHA HODI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI

Na Wazo Huru Blog, Ukerewe-Mwanza

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka Leo Julai 22, 2017 amewasili Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza kwa ziara ya siku moja akitokea Wilaya ya Magu ambapo ndipo ulikuwa mwanzo wa ZIARA yake Mkoani Mwanza.

Katika ZIARA hiyo Ndg Shaka (MNEC) atakutana na makundi ya Vijana, wanachama wa jumuiya zake kufuatia vikao mbalimbali vya chama sambamba na Mkutano utakaofanyika dhidi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Katika ziara hiyo pia Ndg Shaka atazindua mashina ya wakareketwa eneo la Kakukuru, kuzindua Shina la Wakereketwa eneo la Kitanga na baadaye kuhutubia Mkutano Mfupi katika eneo la Kakukuru na Monarch Hotel.

Mara baada ya kuwasili Wilayani Ukerewi na kupokelewa na wenyeji wake Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka pamoja na msafara mzima aliombatana nao walizuru katika Ofisi za CCM Wilaya na kufanya mazungumzo mafupi kabla ya kuelekea mapumzikoni tayari kwa ziara ya kesho.

Ziara hiyo itafanyika kwa siku moja Wilayani Ukerewe ambapo baadaye msafara huo utaelekea Jijini Mwanza kwa maandalizi ya ziara zingine ili kukamilisha ziara ya siku saba katika Mkoa wa Mwanza.

MWISHO.

Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa comrade Shaka Hamdu Shaka akisalimiana na wenyeji wake mara baada ya kuwasili kisiwa cha ukerewe Usiku huu, kwa ziara ya kikazi.(Picha Na Fahad Siraj)

No comments:

Post a Comment