Kaimu Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, leo Julai 22,2017 ameanza ziara ya kikazi ya siku saba mkoani Mwanza.
Mapema asubuhi, Shaka amepokelewa na mwenyeji wake Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza Komredi Mariam Amiry katika ofisi za CCM mkoa wa Mwanza na baadaye kuelekea wilayani Magu ambapo amezindua mashina manane ya vijana wakereketwa wa CCM ambayo ni pamoja na tawi la Nyanguge A na B, Lugeye, Kahangala, Nyigogo, Isandula A na B na pia kushiriki ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Mwamanga pamoja na kuzungumza na wanachama na viongozi wa jumuiya za CCM wakiwemo mabalozi kwenye kikao cha ndani kilichofanyika ofisi za CCM mjini Magu.
Katika maeneo yote aliyopita, Shaka amewahimiza vijana kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kauli mbiu ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya “Hapa Kazi Tu” na kwamba serikali iko tayari kuwaunga mkono katika kutekeleza shughuli zao.
Aidha Shaka amewatahadharisha baadhi ya viongozi katika halmashauri ya Magu ambao wamekuwa wakifanya udanganyifu kwenye mgao wa pesa za vijana zinazotokana na asilimia tano ya mapato ya ndani na kuwata kuhakikisha fedha hizo zinawafikia vijana bila udanganyifu.
Majira ya saa kumi alasiri, Shaka amehitimisha ziara yake wilayani Magu na kuelekea wilayani Ukerewe tayari kwa ajili ya ziara ya kesho wilayani humo.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akivalishwa skafu ya chama baada ya kuwasili ofizi za CCM mkoa wa Mwanza, kwa ajili ya ziara ya kikazi
Mapokezi ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka
Kaimu Kabibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akisalimiana na wanaCCM alipowasili ofisi za CCM mkoa wa Mwanza
Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akizungumza baada ya Kaimu Katibu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka kupokelewa kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mwanza
Katibu wa CCM mkoani Mwanza, Raymond Mwangwala, akitoa salamu zake
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akizindua moja ya shina la vijana wakereketwa wa CCM wilayani Magu
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe.Khadija Nyembo (kushoto), akitoa salamu zake baada ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, kuwasili wilayani kwake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Elisha Hilal (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akifanya uzinduzi wa mashina katika halmashauri yake
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Mwamanga wilayani Magu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akizindua shina la vijana wakereketwa wa CCM wilayani Magu
Mjumbe wa halmashauri Kuu CCM Taifa, kutoka mkoani Mwanza
Viongozi mbalimbali wa CCM
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akizindua shina la vijana wakereketwa wa CCM wilayani Magu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza wilayani Magu
Viongozi mbalimbali wa CCM wilayani Magu wakiwemo mabalozi, wanachama pamoja na viongozi wa jumuiya za CCM wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza nao kwenye ofisi za CCM wilayani humo
Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry akizungumza kwenye kikao cha ndani wilayani Magu
Abdulrahman Kangea mbaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji CCM mkoani Mwanza, akitoa salamu zake kwenye ziara ya Katibu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka mkoani Mwanza
Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Mwanza Ruben Sixtus, akitoa salamu zake kwenye ziara ya Katibu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka mkoani Mwanza
Kaimu Katibu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza wilayani Magu
Credit: www.bmghabari.com
No comments:
Post a Comment