Na Mathias Canal, Misasi-Mwanza
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akiwa mapumzikoni Kijijini kwao Misasi, Kata ya Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza leo 19 Julai, 2017 amefungua mashindano ya mpira wa Miguu kwa wanaume yajulikanayo kama MALONGO CUP 2017.
MASHINDANO hayo yameanza kurindima katika Viwanja vya CCM-Misasi kuanzia Leo Jumatano 19/7/2017 ambapo yanataraji kufika ukomo siku ya Ijumaa Agosti 18, 2017 huku yakitarajiwa kuwa yamewafikia vijana zaidi ya 500 katika Kijiji cha Misasi na vijiji vingine vya jirani.
Akizungumza Wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Vijana wanapaswa kutambua kuwa Michezo inaimarisha Afya, Amani, Umoja na Mshikamano hivyo Mashindano hayo yatakuwa chachu pia katika kuimarisha Undugu na kupunguza matendo ya uhalifu.
Alisema kuwa Vijana wanapaswa kutumia nguvu walizonazo kwa kufanya kazi kwani wao ndio nguvu kazi ya Taifa huku akiwasihi kutojihusisha na matendo maovu ya matumizi ya Dawa za kulevya.
Aidha, Lengo la mashindano hayo ni kuinua vipaji kwa vijana, Kuimarisha mahusiano chanya kwa Vijana sambamba na kuhamasisha Vijana kufanya kazi kwa bidii na kuachana na dhana ya kushinda vijiweni pasina kazi za kufanya.
Katika ufunguzi wa mashindano hayo hii leo imechezwa mechi kati ya Misasi Starz Fc A vs Wega Starz Fc ambapo mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika timu zote zilikuwa zimefungana goli moja kwa moja.
MASHINDANO hayo yanashirikisha timu 13 ambazo ni Timu ya Misasi Starz A Fc, Wega Fc, Inonelwa Fc, Mchongomani Fc, na Manawa Fc
Zingine ni Timu ya Misasi Starz B Fc, Kijama Fc, Nyashimba Fc, Ikungumhula Fc, Mwashilungi Fc, Igobeko Fc, Mwasagela Fc, na Iseni Fc.
Sambamba na hayo pia Mkurugenzi Kayombo ameahidi kutoa shilingi laki moja moja kwa timu zitakazoshika nafasi za juu hususani timu itakayokuwa bingwa, mshindi wa Pili, wa Tatu na Mshindi wa nne. Huku akitoa pia mipira mitatu kwa ajili ya kutumika katika maahindano hayo.
MASHINDANO ya MALONGO CUP 2017 yanadhaminiwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Misasi Ndg Malongo Magese.Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Malongo Cup 2017 yaliyofanyika Kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaMkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Malongo Cup 2017 yaliyofanyika Kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaMkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Wega Fc wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Malongo Cup 2017 yaliyofanyika Kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaMkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Misasi-Misungwi Starz A Fc wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Malongo Cup 2017 yaliyofanyika Kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo akijiandaa kupiga penati kuashiria ufunguzi wa Mashindano ya Malongo Cup 2017 yaliyofanyika Kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaMwenyekiti wa Kijiji cha Misasi Ndg Malongo Magese akisalimiana na wachezaji wa timu ya Wega Fc wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Malongo Cup 2017 yaliyofanyika Kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaWachezaji wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali kutoka kwa mgeni rasmi sambamba na viongozi wa mashindano wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Malongo Cup 2017 yaliyofanyika Kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani MwanzaWachezaji wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali kutoka kwa mgeni rasmi sambamba na viongozi wa mashindano wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Malongo Cup 2017 yaliyofanyika Kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza
No comments:
Post a Comment