Na: Deus Luagila
Hatimae michuano iliyokuwa ikikonga mioyo ya wakazi wa mji wa iringa kama burudani na ajira kwa vijana iliyodhaminiwa na Mh Mbunge Rita Kabati hapo Jana imefikia ukomo huku kinyang'anyiro cha kombe hilo kikitwaliwa na timu ya Ruaha Fc kwa mikwaju ya matuta.
Ikumbukwe kuwa michuano hiyo ilizikutanisha zaidi ya timu 47 mkoani hapo ambapo mshindi wa kwanza aliwekewa zawadi ya pikipiki huku mshindi wa pili akiwekewa zawadi ya kitita cha fedha chenye thamani ya sh,laki tano taslim.
Michuano hiyo ambayo imelindima ndani ya mwezi mzima katika viwanja tofauti-tofauti mkoani hapo jana ilifikia hatamu huku ikizikutanisha timu kati ya Ruaha Fc kutoka wilaya ya iringa na Mucoba Fc ambapo mchezo huo ulichezwa katika viwanja vya kileluu mjini iringa.
Final hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali,wakuu wa wilaya huku mgeni rasim akiwa Mkuu wa mkoa wa Iringa na waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari,
Hata hivyo Taasisi ya kijamii Bunge la jamii lilituma wajumbe wake kwenda kuhudhuria final hiyo na kumtia moyo kiongozi huyo ambae amefanyika kuwa msaada katika taasisi hiyo.
Wingi wa watu waliohudhuria pale lilikuwa ni jibu tosha kuwa huyu Mbunge amefanya jambo la kitofauti kabisa kwa vijana na wakazi wa iringa kwa ujumla.
Mchezo ulichezwa dakika 90 na hakukuonekana bingwa hadi mchezo huo kwenda dk 120 bila ya kupatikana bingwa,ambapo final hiyo iliamliwa kwa mikwaju ya matuta na hatimae Ruaha Fc kuweza kuibuka kidedea katika mikwaju hiyo na kuwa washindi wa Rita Kabati challenge cup 2017.
Mshindi wa kwanza alikabidhiwa kombe na zawadi ya pikipiki huku mshindi wa pili akikabidhiwa fedha taslim laki tano,huku vyombo vya habari vikitunukiwa vyeti vya ushiriki.
Wakiongea kwa nyanja tofauti-tofauti viongozi wa kiserikali walimshukuru Mbunge huyo na kumuomba iwe shughuri endelevu,hata hivyo Mbunge huyo akiwasalim wananchi aliwashukuru kwa ushiriki wao katika shughuri hiyo na kuweka ushirikiano wa kutosha katika mashindano hayo.
Rita Kabati challenge cup ni mashindano ya mpira wa miguu yaliyodhaminiwa na Mh Mbunge Rita Kabati na yalizinduliwa trh 28-05-2017 yakiwa na malengo ya kuwapatia ajira vijana wa kitanzania ili wajikwamue kimaisha,jambo ambalo limefanikiwa kwa wakazi wa iringa.
Kwa niaba ya ofs ya mbunge Rita Kabati,tunawashukuru wote mliojumuika toka mwanzo wa shughuri hii hadi mwisho wa shughuri hii.
Picha na Richard Nnko
No comments:
Post a Comment